AJALI / PICHA:-Taswira Picha Magari 7 ya mizigo na mafuta yaliyokuwa yameegeshwa eneo la Nyakanazi wilayani Biharamulo Mkoani Kagera yalivyoteketea kwa moto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 24, 2015

AJALI / PICHA:-Taswira Picha Magari 7 ya mizigo na mafuta yaliyokuwa yameegeshwa eneo la Nyakanazi wilayani Biharamulo Mkoani Kagera yalivyoteketea kwa moto.

Muonekano wa gLori moja la mafuta likiwa limeteketea kwa moto hapo  jana August 23,2015 likiwa ni kati ya Magari 7 ya mizigo na mengine ya mafuta yaliyokuwa yameegeshwa eneo la Nyakanazi wilayani Biharamulo Mkoani Kagera yakiteketea kwa moto,uliosababishwa wakati watu wakiuziana mafuta.


Mtendaji wa Kata ya Lusahunga Bw Jeremiah Kasaizi amesema tukio hilo limetokea jana August 23,2015 majira ya Saa 4 Usiku na kwamba magari hayo yalikuwa yamebeba Mafuta, Nafaka na Saruji.

Amesema moto huo ulipungua baada ya Jeshi la Zimamoto kufika kutoka mjini Bukoba ambapo hata hivyo halikuwa na vifaa vya kutosha na hivyo wananchi kusaidia kuuzima moto huo kwa kutumia mchanga.

Mmoja wa madereva wa magari hayo amesema hasara iliyopatikana kwenye gari lake ni zaidi ya Sh Milioni 80 na kwamba moto huo umetokea wakati watu wakiuziana mafuta .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Bw Augustino Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba  hakuna mtu aliyefariki bali dereva mmoja amepelekwa kwenye zahanati ya Nyakanazi baada ya Presha kupandaHabari kwa hisani ya RADIO KWIZERA FM








Taswira pichani ya  magari  7 ya mizigo na mafuta yaliyokuwa yameegeshwa eneo la nyakanazi yakiwa yameteketea kwa moto,uliosababishwa wakati watu wakiuziana mafuta .





Wananchi wa  eneo la Nyakanazi ,kata ya Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakishuhudia magari  7 ya mizigo na mafuta yaliyokuwa yameegeshwa eneo hilo yakiteketea kwa moto,uliosababishwa wakati watu wakiuziana mafuta.


PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad