![]() |
|
Bi.Janeth
Magufuli ( Pichani ) bado anasubiri miezi mitatu ya kampeni nzito za kumuwezesha mumewe
kuingia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, lakini walimu na wanafunzi wa Shule
ya Msingi Mbuyuni tayari wanasikitika kumpoteza mwalimu huyo wa jiografia,
historia na Tehama.
Mumewe, Dk
John Pombe Magufuli amepitishwa zaidi ya wiki moja iliyopita kuwa mgombea urais
wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, na hivyo atalazimika kupambana vikali na
wagombea wa vyama vingine ili kujihakikishia anaingia Ikulu kuongoza Serikali
ya Awamu ya Tano.
Iwapo Dk
Magufuli atachaguliwa kuliongoza Taifa Oktoba 25,2015, Shule ya Mbuyuni itakuwa
imeweka historia ya aina yake kwa kutoa wake wawili wa marais.
Bi.Salma
Kikwete, mke wa Rais anayemaliza muda wake, pia alifundisha shule hiyo katika
kipindi chake cha miaka 20 ya utumishi serikalini.
Lakini kitu kingine cha aina yake ni kwamba iwapo Dk Magufuli atakuwa Rais,
maana yake mkewe ataingia kwenye kundi la wake za marais wawili wa nchi zilizo
kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao majina yao ni Janeth.
Mke wa Rais
wa Uganda ni Janet Kataaha Museveni wakati mke wa Rais Paul Kagame wa Rwanda
anaitwa Jeannette Kagame.BOFYA HAPA KUSOMA ZIAIDI....''
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Sunday, July 19, 2015
URAIS TANZANIA 2015:-Mke wa Magufuli awaliza walimu, wanafunzi Mbuyuni.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment