CECAFA KAGAME CUP 2015:-Matokeo ya Leo July 19, 2015 kwa Azam FC na Malakia zikishinda. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 19, 2015

CECAFA KAGAME CUP 2015:-Matokeo ya Leo July 19, 2015 kwa Azam FC na Malakia zikishinda.

Azam FC leo Jumapili wameweza kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya KCCA ya Uganda kwenye mchezo wa kundi B michuano ya Kagame 2015 inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo July 19, 2015.
Bao la ushindi la Azam FC lilifungwa na Straika wao mahiri John Bocco katika Dakika ya 12 baada ya kazi njema ya toka Winga ya Kulia ya Fulbeki Shomari Kapombe aliepanda na kumpa pasi safi.

Mechi nyingine zilizochezwa Leo July 19,2015 ni ile iliyoanza Saa 8 Mchana ya Kundi C  ambapo Malakia ya Sudan Kusini iliifunga Adama City ya Ethiopia Bao 2-1 na kisha Saa 10 Jioni kuchezwa Mechi ya Kundi B huko Karume Stadium ambapo LLB AFC ya Burundi ilitoka 0-0 na Heegan  FC ya Somalia.

Kesho Jumatatu July 20,2015 zipo Mechi mbili, ya kwanza ikiwa ya Kundi A kati ya Telecom ya Djibouti na Khartoum ya Sudan na kisha Mechi ya Kundi A kati ya Gor Mahia ya Kenya na KMKM ya Zanzibar.

MAKUNDI KAGAME CUP 2015.

Kundi A: Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum (Sudan).

Kundi B: APR (Rwanda), Al-Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi), Heegan  FC (Somalia).

Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia), KCCA (Uganda).

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

RATIBA / MATOKEO.

Jumamosi Julai 18,2015.

KMKM 1 – 0 Telecom      
     
APR 1 – 0 Shandy     
    
Yanga 1 – 2 Gor Mahia  
     
Jumapili Julai 19, 2015

LLB AFC 0 – 0 Hegaan FC 

Adama City 1 – 2 Malakia 

Azam 1 – 0 KCCA   
       
Jumatatu Julai 20, 2015

Telecom Vs Khartoum [Saa 8 Mchana] 
     
Gor Mahia Vs KMKM [Saa 10 Jioni] 

Jumanne Julai 21, 2015

Shandy Vs LLB AFC [Saa 8 Mchana] 
     
Hegaan Vs  APR [Saa 10 Jioni]

Malakia Vs Azam [Saa 10 Jioni]  
  
Jumatano Julai 22, 2015

Khartoum Vs KMKM [Saa 10 Jioni]

KCCA Vs Adama City [Saa 8 Mchana]  
    
Telecom Vs Yanga [Saa 10 Jioni]

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad