|
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,
Dk. Ezekiel Mpuya alithibitisha kupokea maiti nane na majeruhi 55.
Alisema
maiti mbili ziliongezeka kutoka kwa majeruhi 55 ambao walikuwa kwenye matibabu.
Alisema
waliokufa wakiwa hospitalini hapo ni mwanamke mjamzito, Rukia Mkupe na Mussa
Kashinde.
Mbali na
hao, wengine ni Elias Mibawa, Mfungo Matutu, Emmanuel Binamungu, Salum
Ramadhan, Nestory Ambloz, Shimba Masungu, Maduhu Lushanga na Charles Mahushi.
Alisema hali
ya majeruhi hao zinaendelea vizuri ambapo 27 wameruhusiwa, huku mmoja akipewa
rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengine 28 wakiendelea
kutibiwa hospitalini hapo.
Akizungumzia
ajali hiyo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Mnyambugha alikiri
kutokea kwa ajali hiyo saa 12:30 jioni.
|
No comments:
Post a Comment