UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-Maneno ya Mbunge James Lembeli alivyotangaza kuhama CCM kwenda CHADEMA leo July 21 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 21, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-Maneno ya Mbunge James Lembeli alivyotangaza kuhama CCM kwenda CHADEMA leo July 21 2015.

Mwaka 2015 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania, kila siku stori za Siasa zimekuwa kwenye masikio ya watanzania wengi kuanzia Magazetini, kwenye TV, Radio na hata mitandaoni.

Mbunge James Lembeli alikuwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili.. kuna stori za baadhi ya Wabunge wametangazwa kuhama Vyama vyao, Lembeli kathibitisha kuhama CCM kwa maneno yake mwenyewe.
James Lembeli akiwa na Mchungaji Peter Msigwa.

>>> ‘Nimetafakari, nimezungumza na mama yangu kwa zaidi ya saa kumi.. mke wangu na watoto wangu, na kwa kusikia kilio cha wananchi wa Jimbo la zamani la Kahama nimeamua kutangaza kuanzia leo Julai 21,2015 kwamba natangaza kujiondoa uanachama wangu ndani ya CCM‘ >>> James Lembeli.

>>>’Nilikipenda lakini nimelazimika kuchukua uamuzi huu, najua nawakera wengi lakini nawaomba waangalie hali ambayo Viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama wamesababisha niamue uamuzi huu mgumu‘>>>

>>> ‘Kuanzia leo Julai 21,2015 najiunga na CHADEMA… Namshukuru Rais Kikwete, nafikiri atakuwa mtu wa kwanza kuamini haya ninayosema, mwaka 2010 mizengwe iliyofanyika lengo lake ilikuwa kukata jina langu, kila mtu anafahamu Rais mwenyewe aliwahi kuniambia lakini Rais Kikwete ndiye aliyerudisha jina langu… Ninaahidi nitaendelea kufanya kazi nae mahali popote, na MUNGU naomba anisaidie niweze kuvuka salama katika haya‘>>>> James Lembeli......IKO HAPA SAUTI YAKE PIA,UKIBOFYA HAPA KISHA PLAY KUMSIKILIZA.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad