NGOMA AFRICA BAND:- Kutumbuiza International African Festival in Tübingen, Ujerumani, Julai 25, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 21, 2015

NGOMA AFRICA BAND:- Kutumbuiza International African Festival in Tübingen, Ujerumani, Julai 25, 2015.

Tübingen,Ujerumani.

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani,inatarajiwa kutingisha jukwaa la
maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni barani ulaya 6th International African Festival in Tübingen, Ujerumani, bendi hiyo maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja  itapanda jukwaani siku ya Jumamosi 27 Julai 2015 majira saa 2.00 Usiku katika uwanja wa Festplatz,Europa str,mjini Tübingen ,uliopo Ujerumani ya Kusini.

FFU-Ughaibuni Jino kwa Jino na Washabiki wa Tubingen Jumamosi 25,07.2017.

Kikosi kazi hiko cha Ngoma Africa Band ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au FFU,chenye utajiri wa wanamuziki vijana waliojaa vipaji, bendi inasadikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani kutokana na mdundo wake "Bongo Dansi" made in Uswahilini.

Bendi hiyo kwa sasa inatamba na CD mpya ya " La Mgambo" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK.
Usikose kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au watupie jicho at www.ngoma-africa.com pia www.facebook.com/ngomaafricaband.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad