|
Gor Mahia
imekuwa timu ya kwanza kutinga kwenye hatua ya robo fainali kwenye michuano ya
Kagame Cup 2015 baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yake miwili kwenye Kundi
A, kundi pekee lenye timu tano kwenye michuano ya Kagame.
Gor Mahia waliibuka
na ushindi wa goli 2-1 kwenye mchezo wao wa ufunguzi kwa kuifunga Yanga SC na leo
Julai 20,2015 wameitwanga KMKM goli 3-1 na kuongoza Kundi A kwa kuwa na pointi sita huku
wakiwa wamefunga magoli matano wakati wao wamefungwa magoli mawili kwenye mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam.
Katika Mechi hiyo, Gor Mahia
walitangulia Dakika ya 3 tu kwa Bao la Meddie Kagere na KMKM kurudisha Dakika
ya 12 kwa Bao la Saimon.
Kipindi cha Pili, Nyota wa Gor Mahia
Michael Olunga, aliipigia Timu yake Bao 2 na kuipa ushindi wa Bao 3-1.
Juzi, Gor Mahia ilianza Mechi zake
za Kundi A kwa kuifunga Yanga Bao 2-1.
Katika Mechi nyingine ya Kundi A
iliyochezwa mapema Leo, Al Khartoum ya Sudan iliitwanga Telecom ya Djibouti Bao
5-0.
Kesho ,Jumanne Julai 21,2015 zipo Mechi mbili za Kundi B
kati ya Al Shandy na LLB AFC Saa 8 Mchana, Uwanja wa Taifa, na kufuatiwa na ile
ya Hegaan vs APR hapo Saa 10 Jioni huko Karume Stadium, wakati Mechi ya
Kundi C kati ya Malakia na Azam itachezwa Uwanja wa Taifa kuanzia Saa 10
Jioni.
MSIMAMO
KAGAME CUP 2015.
Kundi
A
1- Gor Mahia (Kenya) Mechi 2 Magoli
5-2 Pointi 6
2- Khartoum (Sudan) Mechi 1 Magoli
5-0 Pointi 3
3- KMKM (Zanzibar) Mechi 2 Magoli
2-3 Pointi 3
4- Yanga (Tanzania Bara) Mechi 1
Magoli 1-2 Pointi 0
5- Telecom (Djibout) Mechi 2 Magoli
0-6 Pointi 0
Kundi
B
1- APR (Rwanda) Mechi 1 Magoli 1-0
Pointi 3
2- LLB AFC (Burundi) Mechi 1 Magoli
0-0 Pointi 1
3- Heegan FC (Somalia) Mechi 1
Magoli 0-0 Pointi 1
4- Al Shandy (Sudan) Mechi 1 Magoli
0-1 Pointi 0
Kundi
C
1- Malakia (Sudan Kusini) Mechi 1
Magoli 2-1 Pointi 3
2- Azam FC (Tanzania) Mechi 1 Magoli
1-0 Pointi 3
3- Adama City (Ethiopia) Mechi 1
Magoli 1-2 Pointi 0
4- KCCA (Uganda) Mechi 1 Magoli 0-1
Pointi 0
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment