CECAFA KAGAME CUP 2015:-Taswira Picha Azam FC na APR wakienda robo fainali baada ya ushindi katika mechi zao za leo July 21, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 21, 2015

CECAFA KAGAME CUP 2015:-Taswira Picha Azam FC na APR wakienda robo fainali baada ya ushindi katika mechi zao za leo July 21, 2015.

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’

John Bocco ‘Adebayo’ na Kipre Tchetche wameipeleka Azam FC kwenye hatua ya robo fainali baada ya kila mmoja kufunga goli kwenye mchezo wa leo Julai 21,2015 kati ya Azam FC dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya Kagame Cup 2015 ambapo Azam FC ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Bocco alianza kuifungia Azam  FC goli la kuongoza dakika ya 27 kipindi cha kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo nje kidogo ya eneo la hatari la Malakia goli lililoipeleka Azam mapumziko ikiwa mbele kwa goli 1-0 huku   Kipre Tcheche ambaye alifunga goli la pili dakika ya 52 ya kipindi cha pili. 
Huu ni ushindi wa pili kwa Azam katika Mechi zao za Kundi C baada ya Juzi kuifunga KCCA ya Uganda 1-0.

Katika Mechi mbili za Kundi B zilizochezwa pia Leo Julai 12,2015, Al Shandy na LLB AFC zilitoka Sare ya 2-2 na Hegaan kuchapwa 2-0 na APR ambayo nayo ipo Robo Fainali ikibakiza Mechi moja ya Kundi lao.
Kesho Jumatano Julai 22,2015 zipo Mechi 3 lakini macho yote yapo Mechi ya Yanga SC, waliofungwa 2-1 na Gor Mahia, wakicheza na Telecom ya Djibouti, iliyofungwa  1-0 na KMKM na kuchapwa 5-0 na Al Khartoum.

Jumanne Julai 21, 2015

Shandy 2 - 2 LLB AFC   

 
Hegaan 0 - 2  APR 

Malakia 0 - 2 Azam 
    
Jumatano Julai 22, 2015

Khartoum Vs KMKM [Saa 10 Jioni]

KCCA Vs Adama City [Saa 8 Mchana] 
     
Telecom Vs Yanga [Saa 10 Jioni] 

Al hamis Julai 23, 2015

Hegaan Vs Shandy [Saa 8 Mchana]   
   
APR Vs LLB AFC  [Saa 10 Jioni]


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad