Mkutano wa Chama cha ACT
Wazalendo umefanyika Jumanne ya July 21, 2015 mjini Kasulu ,mkoani Kigoma
ambapo pamoja na mambo mengine Wanachama 798 wa Chama cha NCCR Mageuzi wilayani
Kasulu Mkoani Kigoma wamekihama Chama hicho na kujiunga na Chama cha ACT
Wazalendo wakimfuata Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini anayemaliza Muda wake Bw
Moses Machali na Katibu wake Bw Elisha Kabezi.
Wanachama hao wamejiunga na
ACT Wazalendo katika Mkutano wa hadhara wa ACT Wazalendo wilayani humo
uliofanyika kwenye Viwanja vya Kiganamo kwa lengo la Kumpokea Bw Machali na
kumkabidhi kadi ya Chama hicho .
|
No comments:
Post a Comment