![]() |
Picha ya Post iliyopostiwa na Kijana
ajulikanae kama Raffayel Mombury.
Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ni
waandaaji na waendeshaji wa shindano la Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo
kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo linaendelea kufanyika huku washiriki
watano Wakiwa washaenguliwa katika shindano hilo Kutokana na Kutokupata kura za
kutosha kutoka kwa watazamaji wa Kipindi hiko mahiri kinachorushwa na kituo cha
runinga cha ITV siku ya jumapili saa tatu na nusu usiku.
Proin Promotions tunasikitika kusema kuwa kuna
habari ambazo sio za kweli ambazo zimepostiwa katika ukurasa wa facebook wa
kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Raffayel Mombury ambae
amepost taarifa hiyo yenye kichwa cha Habari "WASHIRIKI
WA TMT 2015 WAFUMANIWA WAKINGONOKA" kama inavyoonekana kwenye picha
hapo juu, Sisi kama Proin Promotions ltd tunapenda kusema kuwa taarifa hizo
hazina ukweli wowote na sura hizo hatuzitambui na wala sura zinazoonekana
katika post hiyo sio za washiriki wetu wa TMT 2015 na hazijawahi kuwa.
Kutokana na post hiyo ambayo yenye mlengo wa
kuichafua Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio waandaaji na waendeshaji
wa shindano pamoja na mradi mzima wa TMT ambao unaaminika Tanzania Nzima na Nje
ya Tanzania tumepata usumbufu mwingi kutoka kwa wapenzi wa Shindano hilo pamoja
na wazazi wa Washiriki waliobakia.
Tunapenda kusema kuwa kiukweli taarifa hizo
zimetuletea usumbufu mkubwa sana na kupelekea kuvunja imani kwa watazamaji wetu
na wapenzi wa vipindi vyetu, Sisi kama Proin Promotions tunawaomba Watanzania
na Wapenzi wa TMT kuzipuuza taarifa hizo na hakuna kitu kama hiko
kwasababu Nyumba wanayoishi washiriki wa TMT 2015 imezingatia maadili makubwa na
kuwepo kwa usimamizi wa matron katika kambi hiyo.
Proin promotions tunasema kutokana na taarifa
hizi kutokuwa na ukweli wowote tunaahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
mtu huyu aliyesambaza taarifa hizi za uongo na zilizotuletea usumbufu mkubwa sana
katika jamii inayofuatilia shindano hili na kupelekea kupoteza imani kwa jamii.
Imetolewa na
Idara ya Mahusiano ya Umma
Proin Promotions Ltd.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Thursday, July 23, 2015
TAARIFA KWA UMMA:- Ni Kuhusu Taarifa zisizo na Ukweli dhidi ya Washiriki wa TMT 2015.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment