LIGI KUU TANZANIA BARA 2015 / 2016:- Haya hapa Mabadiliko Mapya sasa kuanza September 12,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 21, 2015

LIGI KUU TANZANIA BARA 2015 / 2016:- Haya hapa Mabadiliko Mapya sasa kuanza September 12,2015.

Mechi ya watani Simba SC na Yanga SC.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza September, 12,2015  badala ya Agosti 22,2015  ili kumpa Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake kuelekea mechi ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria itakayochezwa Sept 5,2015.


Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayozikutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22,2015 badala ya Agosti 15,2015. 

Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa inafanyiwa marekebisho kwa ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine mechi sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya Octoba 25,2015 hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge. 

Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.

Wamiliki wa viwanja vyenye upungufu wameandikiwa barua kutakiwa kurekebisha upungufu katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa kutumika kwa ajili ya PL na FDL.

Timu ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Nyerere uliopo Mbulu mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu uliopo kwenye uwanja huo urekebishwe kwanza.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad