![]() |
|
Mashabiki wa
Gor Mahia wakiwa wanaisapoti timu yao kwa nguvu zote kwenye mchezo wa ufunguzi wa
michuano ya Kagame Cup uliopigwa leo Julai 18,2015 jioni kwenye uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam. |
![]() |
| Kama kawaida ya Yanga na Simba, mashabiki wa Simba wakiiunga mkono timu ya Gor Mahia. |
![]() |
| Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kwa makusudi mchezaji wa Gor Mahia. |
![]() |
|
Yanga walitangulia kupata goli dakika ya nne kipindi cha kwanza kupitia
kwa mshambuliaji wao mpya Donald Ngoma walie msajili kutoka klabu ya FC
Platinum ya Zimbabwe lakini bao hilo halikuweza kudumu kwani Haruna Shakava
aliisawazishia Gor Mahia goli hilo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza na timu
hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana goli 1-1.
Michael Olunga aliifungia Gor Mahia goli la pili dakika ya 45 katika
kipindi cha pili na kuipa ushindi timu yake dhidi ya Yanga, mabingwa wa
Tanzania bara (Yanga) walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha lakini mambo
yalikuwa magumu kwa upande wao.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Gor
Mahia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati akiwa kwenye harakati za
kuokoa shambulizi lililofanywa na Yanga wakati wakilisakama lango la Gor Mahia
wakitafuta goli la kusawazisha.
Nao APR ya
Rwanda imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe
la Kagame kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Katika mchezo huo wa Kundi C, bao pekee la APR lilifungwa na kiungo Bizimana Djihad, dakika ya 64 kwa shuti kali baada ya kupasua katikati ya Uwanja na baada ya kupata upenyo.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|











No comments:
Post a Comment