ARSENAL 3 -1 EVERTON:- Ni Theo Walcott, Santi Cazorla and Mesut Ozil waipa Kombe la Asia mjini Singapore. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 18, 2015

ARSENAL 3 -1 EVERTON:- Ni Theo Walcott, Santi Cazorla and Mesut Ozil waipa Kombe la Asia mjini Singapore.

Washika bunduki wa London, Arsenal wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Asia Trophy baada ya kuichapa Everton mabao 3-1 katika mechi ya fainali iliyopigwa leo Julai 18,2015.

Kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger alikuwa ametulia kwenye benchi huku vijana wake wakionesha kiwango cha hali ya juu katika mechi hiyo ambayo ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya.

Golikipa mpya wa Arsenal aliyesajiliwa kutoka Chelsea majira haya ya kiangazi, Petr Cech amecheza mechi yake ya kwanza na kuokoa michomo ya hatari.

Magoli ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott (22), Saint Cazorla (58) na Mesut Ozil (63).

Bao pekee la Everton limefungwa na Ross Barkley (76) .

Mshambuliaji wa Arsenal, Walcott akiungana na Olivier kushangilia.


Golikipa wa zamani wa Chelsea, Petr Cech amecheza mechi yake ya kwanza.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad