AJALI / MOTO:- Taswira Picha 4 za Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo lilivyoteketea kwa moto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 18, 2015

AJALI / MOTO:- Taswira Picha 4 za Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo lilivyoteketea kwa moto.

Muonekano wa Ofisi  ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma,ikiwa  imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 17,2015  kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo hakuna kitu chochote kilichoweza kuokolewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Judafabrious Mboya akizungumza katika eneo la tukio alisema kuwa ofisi zilizoungua ni pamoja na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Masijala ya wazi, masijala ya siri na ofisi ya utumishi.

Mboya alisema kuwa nyaraka zote na samani zilizokuwa kwenye ofisi hizo zimeteketea kwa moto na kwamba sasa hawajajua thamani halisi ya vitu vilivyotoketea.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo alisema kuwa chanzo cha moto huo ambao ulianza majira ya usiku hakijajulikana.

Mkuu wa Polisi wilaya Kibondo, Marco Joshua alisema kuwa kutokuwepo kwa magari ya zimamoto wilayani humo imekuwa sababu kubwa ya kushindwa kudhibitiwa kwa moto huo.

Hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na moto huo.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad