KAGAME CUP 2015:-Taswira Picha wakati Azam FC wakiimaliza Yanga SC kwa matuta leo July 29, 2015 uwanja wa Taifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 29, 2015

KAGAME CUP 2015:-Taswira Picha wakati Azam FC wakiimaliza Yanga SC kwa matuta leo July 29, 2015 uwanja wa Taifa.

Nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' akimuinua beki Aggrey Morris baada ya kufunga penalti ya mwisho na kuiwezesha timu yao kutinga Nusu Fainali
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM 

Timu ya Azam FC imefanikiwa ‘kuangusha mbuyu’ na kusonga Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kufuatia ushindi wa penalty 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa Aishi Salum Manula aliyepangua penalti ya beki mpya wa kushoto wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali.

Aggrey Morris akaenda kufunga penalti ya mwisho ya Azam FC na kuzima kabisa matarumbeta na shangwe za Yanga SC Uwanja wa Taifa.

Penalti nyingine za Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Serge Wawa Pascal wote raia wa Ivory Coast, John Bocco na Himid Mao, wakati za Yanga SC zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.  
Beki wa Yanga SC, Juma Abdul akigombea mpira dhidi ya kiungo wa Azam FC, Farid Mussa (kulia)
Kikosi cha Yanga SC leo July 29,2015.
Kikosi cha Azam FC leo July 29,2015.

Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' akiulinda mpira dhidi ya Nahodha wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' ili kipa wake, Ally Mustafa 'Barthez' audake
Mshambuliaji wa Yanga SC, Mzimbabwe Donald Ngoma akimiliki mpira mbele ya beki wa Azam FC, Kheri Abdallah


Azam FC sasa itamenyana na KCCA ya Uganda katika Nusu ya pili Ijumaa July 31,2015, baada ya Khartoum N na Gor Mahia kupambana katika Nusu Fainali ya kwanza.

Utamu ni kwamba, Nusu Fainali zote zitakuwa marudio ya mechi za makundi, kwanza Azam FC iliifunga 1-0 KCCA katika mechi ya Kundi C na Khartoum N ilitoka sare ya 1-1 na Gor Mahia katika mchezo wa Kundi A.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad