KAGAME CUP 2015:-Rasmi sasa GOR Mahia dhidi ya Khartoum Nusu fainali huku jioni ya Leo ni Yanga dhidi ya Azam FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 29, 2015

KAGAME CUP 2015:-Rasmi sasa GOR Mahia dhidi ya Khartoum Nusu fainali huku jioni ya Leo ni Yanga dhidi ya Azam FC.

Klabu ya Al Khartoum imeifanyia kitu mbaya APR FC baada ya kuifumua timu hiyo ya Ligi Kuu ya Rwanda mabao 4-0 katika mechi yao ya jana July 28, 2015,kwenye mchezo huo wa uliopigwa majira  alasiri.

 Mechi hiyo ya robo fainali ya kwanza ya Kombe la Kagame mwaka huu 2015 imechezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa kwa mara ya kwanza timu hiyo iliyotinga fainali mbili zilizopita za michuano hiyo, wachezaji wake wakiondoka kwenye uwanja huo kichwa chini.

Kwa matokeo hayo, Al Khartoum itacheza nusu fainali ya Kombe la Kagame Alhamisi  wiki hii July 30, 2015 dhidi ya mshindi kati ya mabingwa wa Kenya, Gor Mahia na Malakia FC ya Sudan Kusini ambao jioni ya leo wanacheza mechi ya robo fainali ya pili kwenye Uwanja wa Taifa.
Robo Fainali nyingine zitachezwa leo July 29, 2015 kati ya Al Shandy Sudan dhidi ya KCCA ya Uganda kuanzia Saa 7:45 mchana na baadaye Azam FC dhidi ya Yanga SC, Uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam.

Nusu Fainali zitafuatia Ijumaa na Fainali pamoja na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu itakuwa Jumapili, siku ya kilele cha mashindano hayo.


Nayo timu ya  GOR Mahia ya Kenya itamenyana na Khartoum N ya Sudan katika Nusu Fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Ijumaa wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hiyo inafuatia Gor Mahia inayofundishwa na Mscotland, Frank Nutal kuifunga mabao 2-1 Malakia ya Sudan Kusini katika Robo Fainali ya pili jioni hii Uwanja wa Taifa, Jijini.


MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA KAGAME 

ROBO FAINALI
Julai 28, 2015
APR (Rwana) 0-4 Khartoum N (Sudan)
Gor Mahia (Kenya) 2-1 Malakia (Sudan Kusini) 
Julai 29, 2015
Al Shandy (Sudan) Vs KCCA (Uganda) (Saa 7:45 mchana)
Azam FC Vs Yanga SC (zote Tanzania) (Saa 10:15 jioni) 
NUSU FAINALI
Julai 31, 2015
Khartoum Vs Gor Mahia (Saa 8:00 mchana)
Al Shandy/KCCA Vs Azam/Yanga (Saa 10:00 jioni)
Agosti 2, 2015 
MSHINDI WA TATU Saa 8:00 mchana
FAINALI Saa 10:00 jioni


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad