|
Mwenyekiti
wa taifa wa Chadema Mh.Freeman Mbowe.
Chama cha
Demokrasia na maendeleo (Chadema) na vyama washirika vinavyounda umoja wa katiba
ya wananchi (UKAWA ) wamesema kuwa wako imara na wamejiandaa vyema kushinda
katika uchaguzi mkuu ujao kwa kukiondoa madarakani chama cha mapinduzi, licha
ya kauli inayodaiwa kutolewa na katibu mwenezi wa chama hicho Nape Nnauye
wakati wa ziara ya katibu mkuu wa chama hicho mkoani Mwanza kwamba CCM
itashinda hata kwa goli la mkono.
Kauli hiyo
imetolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya magomeni
kirumba jijiji Mwanza na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mikoa ya kanda ya
ziwa ambapo katika mkutano huo mwenyekiti wa taifa wa Chadema Mh.Freeman Mbowe
amewatambulisha rasmi waliokuwa wabunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Mh.
James Lembeli na Mh. Esther Bulaya ambao wamehamia Chadema, huku
akiwatahadhalisha wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kutokubali
kununuliwa kwa lengo la kukihujumu chama
hicho.
Awali
mwenyekiti wa taifa wa baraza la wanawake wa Chadema (BAWACHA) Halima Mdee,
naibu katibu mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar Salum Mwalim pamoja na
mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu wamesema wakati umefika kwa watanzania
kuchagua viongozi wanaokubalika na wenye uchungu na raslimali za taifa kwa
uhuru bila kutishwa kwani saa ya ukombozi kupitia sanduku la kura utajulikana
oktoba 25 mwaka huu.
Kwa upande
wao waliokuwa wabunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi James Lembeli wa jimbo
la Kahama na Esther Bulaya viti maalum umoja wa vijana CCM mkoa wa Mara nao
wametumia mkutano huo kueleza kilichowasukuma kujiunga na Chadema.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment