AJALI YA BASI NA GARI-BUKOBA:-Maziko ya Mapadre na Sista kufanyika kesho Al hamisi July 30, 2015 saa tatu asubuhi parokiani Rulenge,wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 29, 2015

AJALI YA BASI NA GARI-BUKOBA:-Maziko ya Mapadre na Sista kufanyika kesho Al hamisi July 30, 2015 saa tatu asubuhi parokiani Rulenge,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Basi la Kampuni ya Sabuni Express lenye namba za Usajili T 950 BFW linalofanya safari zake kati ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na Jiji la Mwanza kugongana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser namba T 169 AJU mali ya Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara, katika ajali  iliyotokea Jana July 28, 2015 Majira ya saa mbili Asubuhi,eneo la Kijiji cha Kagare, kata ya Bugorora wilayani Misenyi Mkoani Kagera na kuua papo hapo Mapadre wawili na Mwanafunzi mmoja wa kidato cha 3,wote kutoka  Seminari ya Katoke wilayani Biharamulo  Kagera na Sista mmoja kutoka Parokia ya Biharamulo.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Augustine Ollomi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo chake ni dereva wa Land Cruser kuendesha bila kuchukua tahadhari hivyo kugongana uso kwa uso na basi la Sabuni.

Aidha Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge –Ngara anasikitika kutangaza vifo vya Mapadre hao, Onesimo Bahabwa (miaka 40 ) na Michael Mwelinde ( 70 ) ,Sr.Magret Kadede ( 60 ) na Mseminarist Everius Kamugisha vilivyotokea jana July 28, 2015 saa mbili asubuhi kwa ajali ya gari.

Amesema maziko ya Mapadre hao na Sista yatafanyika kesho Al hamisi July 30, 2015 saa tatu asubuhi parokiani Rulenge,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi …….Amini.



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad