PICHA / HABARI:-Wauguzi wilayani Ngara mkoani Kagera watakiwa kutumia kauli za kuwafariji Wagonjwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 13, 2015

PICHA / HABARI:-Wauguzi wilayani Ngara mkoani Kagera watakiwa kutumia kauli za kuwafariji Wagonjwa.

Pichani ni Baadhi ya Wauguzi wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa na Bango lenye kuwatakiwa kutumia kauli zenye kuwafariji wagonjwa  wakiwa kwenye vituo vya kutolea huduma hatimaye waweze kuaminiwa na jamii na kuwapa matumaini ya kuishi wagonjwa wao wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi yaliyofanyika kwa kumuenzi Muuguzi mkuu Florence Naitingaly raia wa nchini Italia leo May 13,2015.




Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara Dr  Nelson Rufano (Pichani kulia)  wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi yaliyofanyika kwa kumuenzi Muuguzi mkuu Florence Naitingaly raia wa nchini Italia yaliyofanyika leo May 13,2015, amesema kuwa wauguzi  ndio wanaokaa na wagonjwa muda mrefu na kubaini changamoto zinazowakabili hivyo wakitumia lugha ya upole inaweza kuwatia matumaini wagonjwa na waangalizi wao. 
 
Aidha Mwakilishi wa Muuguzi mkuu wa wilayani Ngara Bi Doroth Ntakamulenga amewahimiza wauguzi hao tawi la Nyamiaga kufanya kazi  bila ya kuomba rushwa kutoka kwa wagonjwa na kuweza  kuaminika ndani ya jamii  .




Kwa upande wao wauguzi wamesema wanafanya kazi katika mazingira magumu lakini wanahita uvumilivu na subira ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya pamoja kuwakemea wanaojitokeza kudhalilisha taaluma yao.

Maadhimisho hayo yaliambatana na Burudani ya muziki kwa wauguzi hao huku baadhi yao wakipatiwa zawadi ya utendaji kazi bora ambapo Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw Patrick Ogo amewataka wauguzi  kujituma na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea bali wajiendeleze kitaaluma.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad