TUME YA UCHAGUZI TANZANIA:-Yasema Uchaguzi mkuu Otober 2015 Hautasogezwa Mbele. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 17, 2015

TUME YA UCHAGUZI TANZANIA:-Yasema Uchaguzi mkuu Otober 2015 Hautasogezwa Mbele.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari leo April 17, 2015  jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic,Gregory Kaijage na kushoto ni Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),Sisti Chriati.

Baadhi ya wandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  jijini Dar es Salaam leo April 17, 2015.  (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na haiwezi kufanya uchaguzi huo usogezwe mbele kutokana na suala hilo kuwa la kikatiba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo April 17,2015 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Wanasiasa amekuwa na kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu wakati suala hilo kuhairisha
uchaguzi halipo katika tume.


Amesema kuwa wanasiasa wametakiwa kuangalia maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi  kwani wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo hayana ukweli wowote. 

Amesema zoezi la kuandikisha kwa Mkoa wa Njombe ambalo  linaisha kesho na kuhamia katika mikoa ya Iringa,Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara ambalo litaanza Aprili 24 mwaka huu 2015.
 
Lubuva amesema wanatarajia kupokea vifaa vya  kuandikisha kwa kuchukua alama za vidole (BVR)1600 ambazo zitafanya kazi katika mikoa hiyo na kuhamia Mikoa ya Dodoma,Mbeya,Katavi pamoja na Rukwa  kuongezeka BVR tena 1600 na BVR 1,152 zitafanya kazi katika mikoa Singida,Tabora,Kigoma pamoja na Kagera na uandikishaji utaanza Mei 2 mwaka huu.

Aidha amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litamalizika Julai mwaka huu hivyo wananchi wajiandae katika kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. 

Jaji Lubuva amesema Rais Jakaya Kikwete anataka amalize ili apumzike hivyo hakuna mpango wowete wa kuongeza muda wa uongozi kwake.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad