PICHA/HABARI:- Watu 18 wamefariki dunia kwa ajali baada ya basi kuacha njia na kutumbukia mtoni Wilayani Rungwe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 17, 2015

PICHA/HABARI:- Watu 18 wamefariki dunia kwa ajali baada ya basi kuacha njia na kutumbukia mtoni Wilayani Rungwe.

Watu 18 kati yao 17 wamefariki dunia  papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya gari dogo la kusafirisha abiria aina ya TOYOTA HIACE  kushindwa kukata kona kali katika eneo la Kiwira wilayani Rungwe Mkoani Mbeya na kupinduka kabla ya  kutumbukia mtoni.

 Gari hilo lenye namba za usajili T290 ABU ambalo limesajiliwa kufanya safari zake kama daladala Jijini Mbeya, leo April 17, 2015,asubuhi limepakia abiria wapatao 20 kwa ajili kuwasafirisha kwenda TUKUYU  wilayani Rungwe na likiwa katika mwendo mkali dereva wake ameshindwa kukata kona kali za ilongobota, eneo lijulikanalo maarufu kwa jina la uwanja wa ndege na kutumbukia katika mto kiwira.

Kaimu Mganga mkuu wa wilaya Rungwe Dk. Aminiel Ngumuo amekiri kupokea miili 17 ambayo imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe,MAKANDANA  na majeruhi watatu ambao  wanatibiwa katika hospitali ya misheni ya Igogwe ambako pia mwili wa majeruhi aliyefariki wakati akipelekwa hospitalini hapo umehifadhiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo chake ni mwendo kasi, huku akiwata madereva kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad