LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Yanga SC na mpango wa Ubingwa wakuhitaji Pointi 6 tu katika Mechi 4 walizobakisha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 22, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Yanga SC na mpango wa Ubingwa wakuhitaji Pointi 6 tu katika Mechi 4 walizobakisha.

Vinara wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara msimu huu 2014/2015, Yanga SC hapo jana April 21,2015 iliifunga kwa tabu  Stand United ya Shinyanga Bao 3-2 wakati wa mchezo wa ligi kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kujihakikishia kuwa moja ya Timu mbili zitakazocheza Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika Msimu ujao.

 Kwa ushindi huo ,Yanga SC sasa wamefikisha Pointi 49 ambazo zinaweza kufikiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC pekee na hii inahakikisha Yanga SC wataweza kucheza Kombe la Shirikisho ikiwa hawatatwaa Ubingwa ambao wanahitaji Pointi 6 tu katika Mechi 4 walizobakisha.

Bingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara huiwakilisha Tanzania Bara kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI na Mshindi wa Pili hucheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.

Mechi inayofuata kwa Yanga SC ni Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

LIGI KUU VODACOM 2014/2015 MSIMAMO.

1. Yanga Mechi 22 Pointi 49

2. Azam FC Mechi 22 Pointi 42

3. Simba Mechi 22 Pointi 35

4. Kagera Sugar Mechi 23 Pointi 31

5. Ruvu Shooting Mechi 23 Pointi 29

6. Mtibwa Sugar Mechi 23 Pointi 28

7. Mbeya City Mechi 23 Pointi 28

8. Mgambo JKT Mechi 22 Pointi 28

9. Stand United Mechi 23 Pointi 28

10. Coastal Union Mechi 23 Pointi 27

11. JKT Ruvu Mechi 23 Pointi 25

12. Ndanda FC Mechi 23 Pointi 25

13. Polisi Moro Mechi 23 Pointi 24

14. Tanzania Prisons Mechi 23 Pointi 22

Simba SC waligoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo walipocheza na Mbeya City jumamosi iliyopita uwanja wa Sokoine.Picha kwa hisani ya  Shaffih Dauda.

Ligi hiyo itaendelea siku ya leo Jumatano April 22, 2015 kwa michezo miwili, Simba SC watakuwa wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Polisi Morogoro wakiwakaribisha Coastal Union katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

LIGI KUU VODACOM/ RATIBA

Jumatano Aprili 22,2015.

Simba SC v Mgambo JKT

Polisi Moro v Coastal Union

Jumamosi Aprili 24,2015.

Ruvu Shooting v Yanga SC 


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

1 comment:

Post Bottom Ad