LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Mabingwa watetezi, Azam FC wamekwaa kisiki nyumbani huku Amisi Tambwe amepiga ‘hat trick’ Yanga SC ikishinda 8-0 Taifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 08, 2015

LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Mabingwa watetezi, Azam FC wamekwaa kisiki nyumbani huku Amisi Tambwe amepiga ‘hat trick’ Yanga SC ikishinda 8-0 Taifa.

VINARA wa Ligi Kuu Vodacom Yanga SC Leo April 8, 2015 , wameitekeza Coastal Union Bao 8-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kupaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa Watetezi Azam FC ambao nao Leo nao wamekwaa mkenge wa Mbeya City baada kutoka nao Sare ya Bao 1-1.

 Huko Uwanja wa Taifa ilikuwa burudani tupu kwa Washabiki wa Yanga ambao Wikiendi iliyopita walisheherekea Timu yao kutinga Raundi ya Pili ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho baada ya kuibwaga FC Platinum kwa Jumla ya Mabao 5-2 katika Mechi mbili.

Amisi Tambwe amefunga manao manne Yanga ikishinda 8-0 leo dhidi ya Coastal Union Ligi Kuu.

Leo Shujaa mkubwa wa Yanga alikuwa Mchezaji wa Burundi Amisi Tambwe aliepachika Bao 4 huku Simon Msuva akipiga Bao 2 na nyingine kufungwa na Mchezaji wa Liberia, Kpah Sean Sherman, likiwa Bao lake la kwanza kwenye Ligi, na jingine na Salum Telela.
Sherman amefuta mkosi kwa kutoa pasi za mabao matatu na kufunga bao moja.

Nao Azam FC, wakiwa kwao Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, walipiga mkenge baada ya kutoka Sare ya Bao 1-1 na Mbeya City inayopigana kujinusuru kutokumbwa na balaa la kushuka Daraja.

Azam FC walitangulia kufunga kwa Bao la Kipre Balou Dakika ya 61 lakini Dakika 4 baadae Mbeya City walisawazisha kwa Penati ya Raphael Alpha.

Matokeo ya Leo yamewafanya Yanga SC wawe juu zaidi kileleni wakiwa na Pointi 43 kwa Mechi 20 na Azam FC wakibaki Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 37 kwa Mechi 19.  

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad