LIGI KUU BARA 2014/2015:-Simba SC na Matumaini ya Ubingwa baada ya Kuifumua 2-1 Kagera Sugar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 06, 2015

LIGI KUU BARA 2014/2015:-Simba SC na Matumaini ya Ubingwa baada ya Kuifumua 2-1 Kagera Sugar.


Klabu ya Simba SC leo April 6, 2015,imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar katika mtanange uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Simba SC ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 49 kipindi cha pili kupitia kwa Ramadhan Singano kabla ya Kagera Sugar kusawazisha kupitia kwa Rashid Mandawa.

Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib aliipachikia timu hiyo goli la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati.

Ibrahim Hajib aliifungia Simba SC bao la pili kwa penalti dakika ya 71, kufuatia Erick Kyaruzi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari katika harakati za kuokoa. 

Hilo linakuwa bao la 10 katika Ligi Kuu msimu huu kwa Mandawa, ambaye sasa amemkamata mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbangu- wote wakiwa nyuma ya winga wa Yanga SC, Simon Msuva anayeongoza kwa mabao yake 11.


Unaweza sema Simba SC sasa wanafufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu 2014/2015, kufuatia ushindi  huo unaowafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 21, ikizidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36, lakini wamecheza mechi 18. Yanga SC wenye pointi 40 za mechi 19, wapo kileleni.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad