CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC rasmi kuvaana na Etoile du Sahel ya Tunisia.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 06, 2015

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC rasmi kuvaana na Etoile du Sahel ya Tunisia.!


Mpinzani wa Yanga SC ya Tanzania kwenye Mashindano ya CAF Kombe la Shirikisho Raundi ya Mtoano ya Timu 16  bora amepatikana Jana April 05,2015 baada ya Mechi ya Marudiano.

Yanga SC sasa wataivaa Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo imeitupa nje Benfica de Luanda kwa jumla ya Mabao 2-1 baada ya kuifunga Mechi ya kwanza 1-0 huko Tunisia na Jana kutoka Sare 1-1 huko Angola.

Yanga SC wamefika Raundi hii kwa kuibwaga FC Platinum ya Zimbabwe Jumla ya Mabao 5-2 baada ya kushinda 5-1 Mechi ya kwanza na kufungwa 1-0 huko Zimbabwe hapo Juzi.

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO.

Raundi ya Mtoano Timu 16 Bora.


Mechi kuchezwa Wikiendi ya Aprili 16,2015.

Al Zamalek v/s  Fath Union Sport de Rabat

Power Dynamos v/s Orlando Pirates 

Association Sportive Olympique de Chlef v/s  Club Africain

Djoliba AC v/s Hearts of Oak

Young Africans v/s  E.S. Sahel

Royal Leopards v/s AS Vita Club

Onze Createurs v/s ASEC Mimosas Abidjan


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad