HALI YA TAHARUKI:-Maiti yenye utata yafukuliwa na kukutwa imekatwa sehemu ya viuongo na sehemu za siri. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 05, 2015

HALI YA TAHARUKI:-Maiti yenye utata yafukuliwa na kukutwa imekatwa sehemu ya viuongo na sehemu za siri.

Hali ya taharuki imewapata wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti ,Kata ya Ikoma wilaya ya Serengeti baada ya Mahakama kutoa ruhusa ya kufukuliwa kwa mwili wa Bi. Celina Jumapili aliyefariki dunia na kuzikwa tarehe March 03,2015 kisha kuonekana utata katika kaburi lake ambalo jana April 4, 2015 limefukuliwa na kukuta sehemu ya viungovya  mwili wake vimekatwa  vikiwemo kiganja cha mguu vidole vya mkono wa kushoto na sehemu za siri zikiwa zimenyofolewa  hali iliyozua mashaka makubwa kwa wakazi wa  kijiji hicho.


Mwandishi wa Habari hizi lifika katika kijiji cha Park Nyigoti wilayani Serengeti na kushuhudia zoezi la kufukua kaburi likiendelea ambapo inadaiwa kuwa marehemu Celina alifariki dunia tarehe 02,March 2015 na kuzikwa tarehe 03,March 2015 lakini tarehe March 22,2015 ,ndugu walikuta sehemu ndogo ya kaburi likiwa limefukuliwa ndipo wakataka kuhakiki kuwa mwili wa ndungu yao upo au umechukuliwa.
Baada ya kupata kibali cha Mahakama wamefukua na kukuta viungo hivyo vikiwa vimekatwa na watu wasiyo julikana.

Akielezea namna tukio ilo lilivyo tokea Mama wa marehemu Celina, Bi Nyahende Kwihamba amesema tukio hilo  limewaweka katika mashaka makubwa kutokana na kijiji hicho kushamiri kwa tabia ya ushirikina na kuiomba serikali isaidie kumaliza tabia hiyo.

Kijiji cha Park Nyigiti mara kwa mara kimekuwa na matukio ya kikatili kwani tarehe mbili ya mwezi marchi  watu watano waliuawa na wananchim kwa kuwatuhumu kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina na tarehe saba ya mwezi wa pili kijiji jirani cha lubanda waliuawa watu wawili na kuchoma moto nyuma saba kwa kama tuhuma hizo hizo.

Source:-Itv.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad