KOMBE LA SHIRIKISHO CAF:-Yanga SC hao 16 Bora dhidi ya Benfica de Luanda au Etoile du Sahel . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 05, 2015

KOMBE LA SHIRIKISHO CAF:-Yanga SC hao 16 Bora dhidi ya Benfica de Luanda au Etoile du Sahel .

Vinara na Mabingwa mara 24 wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara na wawakilishi pekee wan chi ya Tanzania katika mashindano ya kimataifa barani Africa,Yanga SC wakicheza Ugenini Jana April 04, 2015 huko Zimbabwe walifungwa Bao 1-0 na FC Platinum lakini wametinga Raundi ya Pili ya 16 bora ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa Jumla ya Mbao 5-2.


Yanga SC walishinda Mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam Mabao 5-1.
Bao la ushindi la FC Platinum lilifungwa na Water Musoma katika Dakika ya 29.
Kwenye Raundi ya Awali, Yanga SC, ambayo ndio Timu pekee ya Tanzania iliyobaki michuano ya Afrika baada ya Azam FC, KMKM na POlisi ya Zanzibar kutupwa nje, iliibwaga BDF XI ya Botswana kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya kushinda Jijini Dar es Salaam 2-0, kwa Bao za Amisi Tambwe, na kufungwa Mechi ya PIli huko Gaborone 2-1.

Kwenye Raundi ya Pili Yanga SC watakutana na Mshindi kati ya Benfica de Luanda ya Angola na Etoile du Sahel ya Tunisia ambazo zinarudiana leo Jumapili April 5, 2015 huku Sahel ikiwa imeshinda 1-0 katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Tunisia.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad