UEFA na EUROPA 2014/2015:-Zifahamu timu 4 za Nusu Fainali na Droo huru leo April 24, 2015 Kufanyika Mchana. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 24, 2015

UEFA na EUROPA 2014/2015:-Zifahamu timu 4 za Nusu Fainali na Droo huru leo April 24, 2015 Kufanyika Mchana.

Hapo April 22,2015 Klabu Bingwa Ulaya msimu huu 2014/2015  ilikamilisha Mechi zao za Marudiano za Robo Famili na Timu 4 zimetinga Nusu Fainali.

Timu hizo 4 ni Mabingwa Watetezi Real Madrid na wenzao wa Hispania, FC Barcelona, Mabingwa wa Italia, Juventus na Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.

Hapo kesho Ijumaa Aprili 24 Mchana huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu yao, UEFA itaendesha Droo maalum za kupanga Mechi za Nusu Fainali za Mashindano yao makubwa kwa Klabu za Ulaya na Droo hii imeelezwa kuwa ni huru ikimaanisha Timu yeyote inaweza kupangwa na yeyote na hivyo upo uwezekano wa hata kupata El Clasico lile pambano kabambe kati ya Real Madrid na FC Barcelona.

Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13,2015.

Jana April 23, 2015, EUROPA LIGI, Mashindano makubwa ya pili kwa Klabu Barani Ulaya, Usiku wa Alhamisi yamemaliza Mechi zake za Robo Fainali na Mabingwa Watetezi Sevilla ya Hispania, Dnipro Dnipropetrovsk ya Ukraine na Timu mbili za Italia, Fiorentina na Napoli, zimefuzu kuingia Nusu Fainali. 

Mechi za Nusu Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Mei  7 na 14,2015 ni Marudiano.

**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili

Dnipro Dnipropetrovsk 1 – 0 Club Brugge  [1-0]

Fiorentina 2 – 0 Dynamo Kiev  [3-1]

Napoli 2 – 2 VfL Wolfsburg  [6-3]

Zenit St Petersburg 2 – 2 Sevilla2 [3-4]


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad