HONGERA:-Jenerali Muhammad Buhari ndiye Rais mpya wa Nigeria. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 31, 2015

HONGERA:-Jenerali Muhammad Buhari ndiye Rais mpya wa Nigeria.

Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na kumuondoa rais aliyeko Goodluck Jonathan mamlakani kwa ushindi huo wa kihistoria.

 Hii ndiyo mara kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.

Kambi ya Buhari inaongoza kwa asilimia kubwa dhidi ya kambi ya mshindani wake Goodluck Jonathan, na tayari wameanza kusheherekea ushindi.

Mpaka sasa chama cha APC cha Muhammadu Buhari kimepata kura milioni 10.8 katika baadhi ya majimbo ya kaskazini mwa Nigeria, hususan katika majimbo ya Adamawa, Kano na Kaduna, huku chama cha rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan kikipata kura milioni 11.8 Kusini mwa nchi hiyo katika majimbo ya Enugu, Bayelsa na Rivers.

Kwa jumla ya kura zilizohesabiwa Muhammadu Buhari anaongoza kwa kura milioni 15.4 dhidi ya mshindani wake rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan aliyepata kura 13.3.

Duru kutoka Nigeria zimebaini kwamba rais anaye maliza muda wake Goodluck Jonathan amempongeza kwa simu Muhammadu Buhari.

Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Kaskazini mwa Nigeria.

Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, kati ya mwaka 1983-1985.

Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi nchini Nigeria, India, Marekani na Uingereza .

Buhari aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa mfuko wa Amana ya Mafuta. Inasemekana kuwa Buhari ni mtu kaidi, hakubali kushindwa.

Naye rais anayemaliza muda wake Goodluck Jonathan, ni mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini mwa Nigeria.

Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad