Kamishina
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) leo March 31,2015 na hapa …Akisisitiza jambo.
|
Baadhi ya
waandishi wa habari wakimsikiliza Kova kwa makini.
|
Baadhi ya
Askari Polisi wakimsikiliza Bosi wao.
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani
linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka majambazi waliowavamia,
kuwaua askari wawili na kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.
Tukio hilo
limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko barabara ya Kilwa
Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Katika tukio hilo
majambazi wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia
ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi
kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa
Pwani.
Majambazi hao waliwashambulia ghafla askari hao kisha kupora
silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 ndani ya magazine na kutokomea
kusikojulikana.
Majina ya
askari wa Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo:
1.
D.2865
SGT FRANCIS.
2.
E.177
CPL MICHAEL.
Askari
mwenye namba D5573 D/SGT ALLY amejeruhiwa kwa risasi kwenye paja la mguu wa
kushoto na amelazwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu.
Askari huyu
kabla ya kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi hayo kwa kutumia bunduki
aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo walishindwa kumpora hivyo wakatokomea
kuelekea porila Vikindu.
Katika
oparesheni hiyo, nguvu na mbinu zote za kipolisi zitatumika ambapo vikosi vya
Dar es Salaam na Pwani vilianza kufanya oparesheni hiyo mara baada ya tukio ili
kuhakikisha kwamba majambazi hao wanapatikana haraka iwezekanavyo.
Pamoja na
oparesheni hiyo kali inayoendelea, Jeshi la Polisi linachunguza ili kubaini
kama tukio hili linaashiria vitendo vya ugaidi au ni ujambazi wa kutumia
silaha.
Natoa wito
kwa wananchi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kupitia (dhana ya polisi jamii)
kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na mali kwa kutoa taarifa sahihi.
IMETOLEWA
NA:
S.H. KOVA
KAMISHNA WA
POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM
(PICHA
ZOTE NA ISSA MNALLY)
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment