|
Waziri Mkuu wa Tanzania,Bw.Mizengo Pita Pinda.
Mwaka 2012,
Rais Kikwete akiwa ziarani katika mkoa wa Singida, alielekeza kila shule ya
sekondari nchini iwe ina vyumba vitatu vya maabara ifikapo Novemba 30, 2014.
Tangu wakati
huo hadi sasa, utekelezaji unaendelea na kwa mujibu wa Waziri Mkuu, hali ya
ujenzi wa vyumba vya maabara inaonesha hadi Desemba mwaka jana, vyumba 3,607
sawa na asilimia 34 ya mahitaji ya vyumba 10,653 vya maabara nchini vilikuwa
vimejengwa.
Aidha,
vyumba 6,249 sawa na asilimia 59 ya mahitaji, vilikuwa vinaendelea kujengwa na
asilimia saba vilikuwa havijaanza kujengwa. Uchaguzi Mkuu Wakati huo huo Pinda
alisema bajeti ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ni Sh bilioni
218 na ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, ni Sh bilioni 268.
“Naelewa
kwamba changamoto kubwa ni upatikanaji wa fedha hizi kwa muda muafaka. Hata
hivyo, kipaumbele cha Serikali ni kuhakikisha kwamba fedha zinapatikana na kazi
hii muhimu inafanyika kama ilivyopangwa,” alisema.
Kuhusu
Katiba Inayopendekezwa, Waziri Mkuu alitoa mwito kwa wakuu wa mikoa wote
nchini, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu usambazaji wa nakala zake.
Aidha
ametaka wananchi wahimizwe kusoma Katiba hiyo, ili washiriki kikamilifu katika
upigaji kura ya maoni utakaofanyika Aprili 30 mwaka huu.
Source:-Habari Leo.
|
No comments:
Post a Comment