SHERIA YETU:-Taswira ya Picha wakati Bondia Fransis Cheka akienda Jela baada ya Kuhukumiwa Miaka 3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 02, 2015

SHERIA YETU:-Taswira ya Picha wakati Bondia Fransis Cheka akienda Jela baada ya Kuhukumiwa Miaka 3.

Bondia Francis Cheka (kulia) akiwa amepanda ndani ya gari la polisi baada ya kuhukumiwa miaka mitatu jela kwa kumpiga meneja wa baa yake ambapo atamlipa fidia ya sh. milioni moja.

Cheka akiongea jambo wakati akipanda gari la polisi.


Askari Polisi (kushoto) akimwamuru Cheka kutoongea na simu.


Bondia nyota nchini, Francis Cheka ‘SMG’ amehukumiwa miaka mitatu jela katika Mahakama ya  mkoani Morogoro leo Februari 02,2015.

Taarifa zinaeleza Cheka amepatikana na hatia ya kushambulia baada ya kumpiga aliyekuwa Meneja wa baa yake.

Pamoja na kifungo cha miaka mitatu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakamani hiyo, Said Msuya amemhukumu Cheka kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.

Cheka amepatikana na hatia ya shambulio dhidi ya aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda aliyemshambulia Julai 2, mwaka jana, katika Ukumbi wa Vijana Social aliokuwa ameukodi kwa ajili ya kuendesha shughuli za baa zilizokuwa zinasimamiwa na Kibanda.

Kutokana na kukutwa na hatia, Cheka amekuhukumiwa kwenda jela kwa muda huo na imeelezwa tayari ameshapelekwa kwenye gereza mkoani humo.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad