Aidha Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la
10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235,227 sawa na 58.25
walifualu.
Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo Februari14,2015 jijini
Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles
Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61
wakati wavulana ni 106,960.
Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67. Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013. Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33. Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24. Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013. Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58. Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule. Akizitaja SHULE 10 BORA KWA UFAULU NI , Dkt Msonde amesema shule hizo nipamoja na :- Kaizirege mkoa wa Kagera
Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
Marian Boys mkoa wa Pwani
St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
Abbey mkoa wa Mtwara
Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
Marian Girls mkoa wa Pwani
Feza Boys mkoa wa Dar es laam.
SHULE 10 ZA MWISHO NI PAMOJA NA:- Manolo mkoa wa Tanga Chokocho mkoa wa Pemba Kwalugulu mkoa wa Tanga Relini mkoa wa Dar es salaam Mashindei mkoa wa Tanga Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma Vudee mkoa wa Kilimanjaro Mnazi mkoa wa Tanga Ruhembe mkoa wa Morogoro Magoma mkoa wa Tanga. Dkt Msonde pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni:- Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys. | |
Saturday, February 14, 2015
Home
HABARI
MATOKEO YA KIDATO CHA NENE 2014 :-Haya Hapa Yametoka leo Februari 14,2015....Soma Ufaulu wake.
MATOKEO YA KIDATO CHA NENE 2014 :-Haya Hapa Yametoka leo Februari 14,2015....Soma Ufaulu wake.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment