MAFANIKIO:-Yaliyojiri Picha na Hotuba wakati CCM ikiadhimisha Miaka 38 ya kuzaliwa Leo Februari 01,2015 mkoani Ruvuma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 01, 2015

MAFANIKIO:-Yaliyojiri Picha na Hotuba wakati CCM ikiadhimisha Miaka 38 ya kuzaliwa Leo Februari 01,2015 mkoani Ruvuma.


Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo Februari 01,2015 kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.Picha na Ikulu.


Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa viongozi mbali mbali wa CCM wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo Februari 01,2015 kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na kijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikwagua gwaride la chipukizi. Sherehe hizo pia zimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali na kupambwa na gwalide la vijana wa chipukizi na burudani mbalimbali. 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wakati akiingia kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


Vijana wakiangalia picha ya Hayati Abeid Aman Karume ,Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongoza shughuli wakati wa maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM ambayo kitaifa yamefanyika Songea mkoani Ruvuma.




Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo Februari 01,2015 katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM na  amesema kuwa katika kipindi cha miaka 38 tangu kuzaliwa kwa chama hicho Februari 05, 1977. kinajivunia mafanikio makubwa waliyo yapata hususani katika kudumisha masuala ya amani na utulivu.

Akizungumza katika sherehe hizo ,Rais Kikwete amesema amani na utulivu uliopo hapa nchini unaendelea kukifanya chama cha mapinduzi kiendelee kuaminiwa na kutumainiwa na watanzania kama ilivyo thibitishwa katika chaguzi zote tangu mfumo wa vyama vingi ulivyo anza mwaka 1992.

Aidha Rais Kikwete amezungumzia masuala ya katiba ambapo amewataka watanzania kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kura za maoni na kufafanua kuwa inawezekana rais ajaye asilitilie maanani suala la katiba na hivyo kubakia na katiba iliyopo sasa jambo ambalo si jema kwa taifa letu na maendeleo kiujumla.
 


Msanii Diamond akiwaburudisha maelfu ya watu waliofurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM ambazo kitaifa zimeadhimishwa mkoani Ruvuma.

Msanii Diamond akipongezwa na chipukizi wa UVCCM baada ya kutumbuiza katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.


Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo Februari 01,2015 ,katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM. PICHA NA IKULU.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad