|
Mabingwa wa kombe
la Mataifa ya Africa, AFCON 2015 ni Ivory Coast, Dunia nzima ilishuhudia usiku
wa Februari 08,2015,Jumapili huko Estadio de Bata, Mjini Bata Nchini Equatorial
Guinea, Ivory Coast waliibuka Bingwa wa Mataifa ya Afrika kwenye Mechi ya
Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, walipoibwaga Ghana kwa Mikwaju ya Penati 9-8
kama walivyofanya Mwaka 1992.
Hii ni mara
ya pili kwa Ivory Coast kutwaa Ubingwa wa Afrika na mara ya kwanza ni Mwaka
1992 walipoitoa Ghana pia kwa Mikwaju ya Penati 11-10 baada ya suluhu ya 0-0.
Hii pia ni
mara ya pili kwa Kocha wa Ivory Coast, Herve Renard, kutwaa Ubingwa wa Afrika
na mara ya kwanza ilikuwa 2012 alipoiwezesha Zambia kutwaa Ubingwa, tena kwa
kuifunga Ivory Coast, na sasa kuweka Rekodi ya kuwa Mtu wa kwanza kutwaa
Ubingwa wa Afrika na Nchi mbili tofauti.
Kwa Kocha wa
Ghana, Avram Grant, hii ni mara ya pili kushindwa Fainali kubwa kwa Mikwaju ya
Penati baada ya Mwaka 2008, akiwa na Chelsea, alipobwagwa kwa Mikwaju ya Penati
na Manchester United kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Moscow, Urusi.
Rais wa
Ivory Coast, Alassane Ouattara aliongozana na maelfu ya mashabiki ambao
walifurika kwenye mapokezi ya Mabingwa hao baada ya kuwasili nyumbani kwao.
Hapa ni
baadhi ya PICHA za Mabingwa hao baada ya Kukabidhiwa kombe lao na wakati
wakiwasili nyumbani kwao. |
No comments:
Post a Comment