CAF KOMBE LA SHIRIKISHO.:-Yanga SC yasonga mbele,watacheza na Mshindi kati ya Platinum au Sofapaka . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 28, 2015

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO.:-Yanga SC yasonga mbele,watacheza na Mshindi kati ya Platinum au Sofapaka .

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao dhidi ya BDF katika mchezo wa jana lililofungwa na Mrisho Ngassa dhidi ya BDF wa Kombe la Shirikisho barani Afrika uliochezwa jana mjini Gaborone, Botswana. BDF ilishinda mabao 2-1. Picha na Khatimu Naheka .

  Huko Gaborone, Botswana hapo Jana Februari 27,2015, Yanga ilifungwa Bao 2-1 na BDF XI kwenye Mechi ya Pili ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho lakini wamesonga na kutinga Raundi ya Kwanza kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza 2-0 Mjini Dar es Salaa.

Kwenye Mechi ya Jana, Yanga walitangulia Bao 1-0 hadi Mapumziko alilofunga Mrisho Ngassa lakini BDF XI Kipindi cha Pili walifunga Bao 2 na Gemu kwisha 2-1 huku Yanga pa wakiwa Mtu 10 baada ya Danny Mrwanda kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 70.

BDF XI pia walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 21 baada ya Mchezaji wao Mparithe kutolewa kwa Kadi Nyekundu.

Katika Raundi ijayo, Yanga watacheza na Mshindi kati ya Platinum ya Zimbabwe na Sofapaka ya Kenya ambao wanarudiana Wikiendi hii huku Platinum wakiwa washindi wa Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Nairobi.

Leo,Jumamosi Februari 28,2015, Timu nyingine mbili za Tanzania, Azam FC na KMKM, zitakuwa Viwanjani kwenye Mechi zao za Pili za Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONS LIGI wakati Polisi ya Zanzibar itacheza Mechi yake ya Pili ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho hapo Jumapili.

MICHUANO KLABU AFRIKA.

Raundi ya Awali-Mechi za Marudiano
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

CAF CHAMPIONZ LIGI

Jumamosi Februari 28,2015.

El Merreikh [Sudan] v Azam FC [0-2]

KMKM v Al Hilal [Sudan] [0-2]

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO.

Ijumaa Februari 27,2015.

BDF IX 2 Yanga 1 [2-3] === Yanga SC imesonga

Jumapili Machi 1,2015.

Polisi v CF Mounana [Gabon] [0-5]

Azam FC wanahitaji Sare, au hata kufuungwa Bao 1-0, ili kusonga, Timu za Zanzibar, KMKM na Polisi, zinahitaji ushindi mzito ili kupindua matokeo mabaya ya Mechi zao za kwanza walizocheza Ugenini.
 

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad