|
Mananasi
husaidia kutibu vidonda na uvimbe.
Moja kati ya
vurutubisho vilivyoko ndani ya nanasi kinaitwa Bromelain, husaidia sana
kuondoa maumivu kwenye viungo, kupunguza hali ya uvimbe kwenye tezi na
hata kupunguza uvimbe wa kawaida ambao umetokea ndani ya mwili na pia humsaidia
sana mtu akiwa amefanyiwa upasuaji.
Mananasi
husaidia Mfumo wa usagaji (Mmeng’enyo) wa chakula.
Manansi yana
virutubisho vya kambakamba (fibre) ambavyo husaidia sana kwenye kusagwa
kwa chakula mwilini, kirutubisho cha Bromelain pia husaidia kwneye
kusaga chakula tumboni kwa kusaidia kuvunja vile vipande vya protini.
Manufaa
ya nanasi kwenye ngozi.
Vitamini
C ipatikanayo kwenye
mananasi husaidia sana kuipa ngozi mng’ao ambao unahitajika, mishipa midogo ya
damu pia hufaidika sana kutokana na mananasi pamoja na viungo vingine vya mwili
na mifupa pia.
Manufaa
ya nanasi kwenye mifupa.
Mananasi
yana madini aina ya Manganese ambayo husaidia kuzalisha nishati mwilini
huku ikisaidia kutoa ulinzi kwa seli za mwili wa mwanadamu.
Madini haya
yanasaidia sana ufanyaji kazi wa madini mengine na virutbisho kama Thiamine
na Biotin ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia kufanya mifupa kuwa migumu
na yenye afya zaidi na pia husaidia kuyayusha vyakula vyenye mafuta.
Mananasi
husaidia Macho .
Tunda aina
ya nanasi lina vitamin A pamoja jna kirutubisho aina ya Beta-Carotene
ambavyo kwa pamoja husaidia mfumo wa kinga ya mwili na afya ya macho.
Mananasi
hutoa nguvu na nishati na kushusha shinikizo la damu.
Mananasi ya
kiwango kikubwa cha Vitamini B1 na B6 ambavyo ni vyanzo muhimu
sana vya nishati pamoja na kuvunjavunja sukari kwenye mfumo wa usagaji wa
chakula.
Madini ya
shaba pia yanapatikana kwenye mananasi yanasaidia sana kutoa afya kwa seli
nyekundu zinazosaidia kutengeneza damu na madini ya potasia ambayo yanasaidia
kuweka mapigo ya moyo sawa na kushusha shinikizo la damu.
Source:-Millardayo.
|
No comments:
Post a Comment