WAZIRI WA NISHATI NA MADINI :-Taswira ya ziara yake mkoa wa Simiyu kukagua Miradi na Kuzungumza na Wananchi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 06, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI :-Taswira ya ziara yake mkoa wa Simiyu kukagua Miradi na Kuzungumza na Wananchi.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

 Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad