Kamanda wa
Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (Trafic), Mohamed Mpinga (pichani),
ametoa onyo kwa baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza
taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani
yake.
Kamanda
Mpinga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi
wa habari kuhusu tukio la baadhi ya mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na
basi la Kampuni ya Dar Express limepata ajali.
Alisema,
onyo hilo linatokana na kitendo cha baadhi ya mitandao hiyo, jana kusambaza
taarifa kuwa kulitokea ajali iliyohusisha gari namba T 640 AXL,
huku ikishindwa kutoa ufafanuzi ilikotokea jambo ambalo limezua taharuki kwa
abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.
Mitandao
iliyohusika katika kusambaza picha za ajali hiyo ya uzushi ni Bongo Mzuka,
Whatsapp, Facebook na Jamii Forum.
“Baada ya picha ya basi hilo kusambazwa katika mitandao hii nilipigiwa
simu na baadhi ya watu wakitaka kujua kama ni kweli kulikuwa na ajali kama
hiyo, iliwaweze kujua majaliwa ya ndugu zao walio kuwa safarini wakitumia
mabasi ya kampuni hiyo,”alisema Mpinga.
Mpinga, aliwatoa hofu wananchi kuwa hakuna ajali yeyote iliyotokea ambayo
ilihusisha basi la kampuni hiyo katika siku za hivi karibuni na kwamba gari
lililooneshwa katika mitandao ni la uongo kwa vile haliko barabarani.
|
No comments:
Post a Comment