KOMBE KONGWE DUNIA FA CUP:-Historia yake ya maajabu kwa kishindo kikubwa Januari 24,2015 baada ya Vigogo wa Ligi Kuu Uingereza kutupwa nje na ‘Timu ndogo’….Tazama Matokeo hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 25, 2015

KOMBE KONGWE DUNIA FA CUP:-Historia yake ya maajabu kwa kishindo kikubwa Januari 24,2015 baada ya Vigogo wa Ligi Kuu Uingereza kutupwa nje na ‘Timu ndogo’….Tazama Matokeo hapa.

Mechi za kuwania Kombe la FA ,Jana Januari 24,2015,limewafanya mashabiki wa soka Duniani  kushuhudia Maajabu baada ya Vigogo wa Ligi Kuu soka Uingereza, Mabingwa Watetezi Manchester City, Vinara wa Ligi hiyo 2014/2015 , Chelsea, Tottenham na Southampton wote kutupwa nje na ‘Timu ndogo’ nyingine za Daraja la chini tena wote Vigogo hao wakiwa wanacheza Viwanja vya Nyumbani kwao.

 Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea waliongoza Bao 2-0 lakini Bradford City, inayocheza Ligi 1 ikiwa ni Madara mawili chini ya Chelsea, ilizinduka na kupiga Bao 4.
Chelsea walitangulia kwa Bao za Garry Cahill na Ramires na Stead kuipa Bao 1 Bradford kabla ya Kipindi cha Kwanza kumalizika.
Kipindi cha Pili, Bradford walipiga Bao 3 kupitia Morais, Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Halliday na Yeates.       

Huko uwanja wa Etihad, Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Uingereza, Manchester City, walipigwa Bao 2-0 na Middlesbrough inayocheza pia Daraja la chini Championship kwa Bao za Kipindi cha Pili za Bamford na Garcia Martinez.

Nao Tottenham, wakicheza kwao White Hart Lane, walipigwa Bao 2-1 na Leicester City ambao walitoka nyuma kwa Penati ya Andros Townsend ya Dakika ya 19 na wao kupiga Bao mbili katika Dakika ya 83, Mfungaji akiwa Ulloa, na Dakika ya 90 kwa Bao la Schlupp.

Southampton, Timu ambayo iko Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu , ilichapwa Bao 3-2 na Crystal Palace ambayo iko Nafasi ya 13 kwenye Ligi hiyo.

Bao za Mechi hiyo zilifungwa zote Kipindi cha Kwanza na kwa Southampton kuitia Pelle, Dakika ya 9, na Dann, aliejifunga mwenyewe Dakika ya 16 huku Palace wakifunga kupitia Chamakh, Dakika ya 11 na 39, na Yaya Sanogo, Dakika ya 21.

Katika Mechi ya kwanza kabisa , iliyochezwa Ewood Park, Wenyeji Blackburn Rovers, wanaocheza Daraja la chini la Championship, walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuibwaga Swansea City inayocheza Ligi Kuu Bao 3-1.

FA CUP  RAUNDI YA 4.

Ratiba/Matokeo-Ijumaa Januari 23,2015.

Cambridge United 0 – 0  Manchester United 

Jumamosi Januari 24,2015.

Derby 2 – 0 Chesterfield 

Preston North End 1 - 1 Sheffield United 

Birmingham City 1 – 2 West Bromwich Albion 

Cardiff City 1 – 2 Reading 

Sunderland 0 – 0  Fulham 

Manchester City 0 – 2 Middlesbrough 

2030 Liverpool 0 – 0  Bolton Wanderers

Jumapili Januari 25,2015.

1700 Bristol City v West Ham

Jumatatu Januari 26,2015.

2300 Rochdale v Stoke City

1800 Aston Villa v Bournemouth

1900 Brighton & Hove Albion v Arsenal

TAREHE ZA RAUNDI.

-Raundi ya 4: 24 Januari 2015

-Raundi ya 5: 14 Februari 2015

-Raundi ya 6: 7 Machi 2015

-Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015

-Fainali: 30 Mei 2015

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad