|
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw.Zitto Kabwe.
Kuanzia
Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba,2014, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka
kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa.
Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40%
haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na
kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua.
Leo bado bei
ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli,
bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.
EWURA,
inasemekana, wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu
waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo
la bei.
Hata hivyo
bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa
wananchi. Ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na
sababu za kununua ' bulky' huwa hazitolewi.
Ni kweli
kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo.
Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo
ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue.
Vile vile ni
kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi
hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za
kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu.
Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta
ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%.
Katika hali
ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya
mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.
Ni dhahiri
mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za
mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia.
Wananchi
wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo, basi bei hizo zishuke na wananchi
wafaidike na punguzo hilo.
Zitto Kabwe, Mb.
|
No comments:
Post a Comment