FA CUP 2014/2015:- Mabingwa Watetezi Arsenal na Chelsea watinga Raundi ya 4.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 05, 2015

FA CUP 2014/2015:- Mabingwa Watetezi Arsenal na Chelsea watinga Raundi ya 4.!

Mabingwa  Watetezi Arsenal wametinga Raundi ya 4 ya FA CUP baada ya kuichapa Hull City Bao 2-0 Uwanjani Emirates.

Hull City ndiyo Timu ambayo Arsenal waliichapa Mwezi Mei Mwaka Jana na kutwaa FA CUP.
 
Nao Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge, waliichapa Watford, Timu ya Daraja la chini la Championship, Bao 3-0.

Bao za Chelsea zilifungwa zote Kipindi cha Pili na Willian, Loic Remy na Kurt Zouma.

Mabingwa Arsenal walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 20 na Per Mertesacker alipounganisha kwa Kichwa Kona na la pili kufungwa Dakika ya 82 na Alexis Sanchez alieingizwa Dakika ya 76 kumbadili Oxlade-Chamberlain.
Timu zilizosonga Raundi ya 4 ya FA CUP zitajua Wapinzani wao wa Raundi hiyo leo January 5, 2015,Usiku baada ya Droo.

PATA RATIBA/MATOKEO.

Jumapili Januari 4,2015.

Dover 0 Crystal Palace 4  

QPR 0 Sheffield United 3  

Sunderland 1 Leeds 0  
     
Aston Villa 1 Blackpool 0  

Man City 2 Sheffield Wednesday 1  
      
Southampton 1 Ipswich 1 

Stoke 3 Wrexham 1

Yeovil 0 Man United 2

Chelsea 3 Watford 0    
     
Arsenal 2 Hull 0   
  
Jumatatu Januari 5,2015.

2245 Burnley v Tottenham

2255 Wimbledon v Liverpool 
     
Jumanne Januari 6,2015.

2245 Everton v West Ham

2245 Scunthorpe v Chesterfield

TAREHE ZA RAUNDI.

-Raundi ya 3: 3 Januari 2015

-Raundi ya 4: 24 Januari 2015

-Raundi ya 5: 14 Februari 2015

-Raundi ya 6: 7 Machi 2015

-Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015

-Fainali: 30 Mei 2015
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad