SHAMBULIZI UFARANSA:- Taswira ya Picha Yaliyojiri wakati Maandamano makubwa yakifanyika Ufaransa kupinga ugaidi Januari 11,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 12, 2015

SHAMBULIZI UFARANSA:- Taswira ya Picha Yaliyojiri wakati Maandamano makubwa yakifanyika Ufaransa kupinga ugaidi Januari 11,2015.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameongoza maelfu ya watu (Pichani) kwenye mitaa ya Paris Jumapili Januari 11,2015 , katika maandamano makubwa ya kuonyesha umoja na waathiriwa wa shambulizi la kigaidi la Januari 7 lililouwa watu 17.

Rais wa ufaransa Francois Hollande akiwa amezungukwa na viongozi wa dunia kwenye maandamano katika mitaa ya Paris.

Viongozi wa dunia waliungana na Bwana Hollande katika mji mkuu wakati kundi la watu likihamasisha umoja kwenye maandamano kote katika mitaa.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron , kansela wa Ujerumani Angela Markel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas pamoja na mfame na mama mfalme wa Jordan pia walishiriki katika maandamano hayo.


Waziri mkuu wa Uingereza akiwa na Rais wa Ufaransa wakati wa maombolezo Jana Jumapili Januari 11,2015.

Maafisa wa Ufaransa wameita mauaji ya Januari 7,2015, katika ofisi za Paris kwenye gazeti la Charlie Hebdo na mfululizo wa mashambulizi mengine ya mauaji ni ya kigaidi.

Wakati huo huo mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder alitangaza kutoka Paris Jumapili kwamba rais Barack Obama atakaribisha viongozi wa dunia mjini Washington, February 18 katika mkutano wa kupinga ghasia zenye msimamo mkali.

Kushoto ni Chancellor wa Ujerumani akiwa na Hisia kali wakati wananchi wa Ufaransa wakikusanyika kwa pamoja Kuomboleza.





UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad