LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Simba SC V/s Azam FC zagawani alama Leo Januari 25,2015 kupitia Okwi na Tchetche. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 25, 2015

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Simba SC V/s Azam FC zagawani alama Leo Januari 25,2015 kupitia Okwi na Tchetche.

Washambuliaji, Emmanuel Okwi wa Simba SC (kushoto) na Kipre Tchetche wa Azam FC (kulia) wakipambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Januari 25,2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

 Timu hizo zilitoka sare ya 1-1, bao la Simba SC akifunga Okwi kipindi cha kwanza na la Azam FC Kipre Tchetche kipindi cha pili. 

Huko Mjini Mbeya, Uwanja wa Sokoine, Dabi ya Jiji hilo ilimalizika kwa Sare ya Bao 2-2 wakati Mbeya City ilipovaana na Tanzania Prisons.

Nao Mtibwa Sugar, ambao walikuwa hawajaonja kipigo Msimu huu kwenye Ligi, Leo hii Januari 25,2015 wamechapwa 2-1 Ugenini na Ruvu Shooting.

Matokeo haya ya Leo yamewabakisha Azam FC kileleni mwa Msimamo wa Ligi wakiwa na alama 21 kwa Mechi 11 wakifuatiwa na Yanga SC wenye alama 18 kwa Mechi 10 na kisha Mtibwa Sugar wenye Pointi 17 kwa Mechi 10 pia  huku Simba SC ikiwa na alama 13.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad