|
Kikosi
cha Simba sc kilichoanza Usiku wa jana January 05,2015.
Wekendu wa
Msimbazi Simba SC jana January 05,2015, imefuzu Robo Fainali ya Kombe la
Mapinduzi 2015, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi JKU katika mchezo wa Kundi C,
uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Matokeo hayo yanaifanya Simba SC imalize kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake Sita baada ya mechi tatu, mbele ya Mtibwa Sugar iliyomaliza na pointi tano. Simba SC katika mchezo huo walipata bao hilo, lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ dakika ya 12 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi baada ya kupewa pasi nzuri na Said Ndemla. Sifa zimuendee mshambuliaji Mganda, Dan Sserunkuma ambaye baada ya kupewa pasi na kiungo Jonas Mkude, aliwahadaa wachezaji wa JKU kabla ya kumpasia Ndemla aliyempa mfungaji.
Kikosi
cha JKU kilichoanza jana .
Baada ya mechi hiyo, kocha Kopunovic
amesema timu yake inaimarika kidogo kidogo na ilicheza tofauti kwa vipindi
vyote.
“Hii ni siku
ya tano tu tangu nifike, bado naendelea kuwapa mbinu mpya. Wachezaji
wangu kimbinu nawaona wazuri”-“Mimi napenda vijana ndio maana nawatumia wengi.
Kidogo kidogo tutakuwa safi” Alisema Kopunovic.
Simba SC
wanasubiri mpinzani wao wa Robo fainali katika mechi za Leo ambapo kutakuwa na
mechi nne.
Majira ya
saa 9:00 alasiri katika uwanja wa Amaan, KCC watachuana na KMKM, saa 11:00
jioni Azam FC watakabiliana na Mtende, hizo ni mechi za kundi B.
Kundi A,
Taifa ya Jang’ombe itapepetana na Polisi katika uwanja wa Mao Dze Tung majira
ya saa 9:00 alasiri.
Mtanange
mwingine wa kundi A utawakutanisha Yanga SC dhidi ya Shaba majira ya saa 2:00
usiku uwanja wa Amaan.
|
Tuesday, January 06, 2015
KOMBE LA MAPINDUZI 2015:-Simba SC yafuvu Robo Fainali kwa bao la Singano.
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.





No comments:
Post a Comment