AFCON 2015:-Ni Wenyeji Equatorial Guinea na Congo Robo Fainali baada za kuzitoa Gabon na Burkina Faso Januari 25,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 26, 2015

AFCON 2015:-Ni Wenyeji Equatorial Guinea na Congo Robo Fainali baada za kuzitoa Gabon na Burkina Faso Januari 25,2015.

KUNDI A la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, Jana Januari 25,2015 Usiku lilicheza Mechi zao za mwisho na Wenyeji Equatorial Guinea na Congo kufuzu kutinga Robo Fainali baada za kuzitoa Gabon na Burkina Faso.


Gabon, ikiongozwa na Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang, Mchezaji wa Borussia Dortmund, walichapwa Bao 2-0 na Equatorial Guinea Wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, na kubwagwa nje wakati Wenyeji hao wakitinga Robo Fainali kutoka Kundi A.

Kwenye Dakika ya 55, Lloyd Palun wa Gabon alimwangusha Javier Balboa ndani ya Boksi na Refa kuamua ni Penati iliyofungwa na Balboa mwenyewe.

Kinda anaechezea Valencia huko Spain, Iban, aliwapa furaha kubwa Wenyeji Equatorial Guinea kwa kuwafungia Bao la Pili katika Dakika ya 87 baada ya Javier Balboa kumpasia Emilio Nsue ambae Shuti lake liliokolewa na kumfikia Iban aliemalizia.

Nao Congo wametinga Robo Fanali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1992 bada ya kuichapa Burkina Faso Bao 2-1 katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi A la AFCON 2015 huko Mjini Ebebiyin Nchini Equatorial Guinea.

Congo walikwenda mbele Dakika ya 52 baada ya Ferebory Dore kumlisha Thievy Bifouma ambae alifunga Bao kwa Congo na Burkina Faso kusawazisha Dakika ya 86 kupitia Aristide Bance lakini Dakika 1 baadae Congo wakaenda Bao 2-1 mbele kwa Goli la Fabrice Ondama baada Kipa Germain Sanou kuokoa Mpira kwa ngumi na kumgonga Ondama Begani na kutinga.

RATIBA:**Saa za Bongo

Jumatatu Januari 26

KUNDI B

2100 Congo DR v Tunisia [Estadio de Bata]   
            
2100 Cape Verde Islands v Zambia [Nuevo Estadio de Ebebiyín] 
              
Jumanne Januari 27

KUNDI C

2100 South Africa v Ghana [Estadio de Mongomo] 
   
2100 Senegal v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo] 
   
Jumatano Januari 28

KUNDI D

2100 Cameroon v Côte d'Ivoire [Nuevo Estadio de Malabo]   
         
2100 Guinea v Mali [Estadio de Mongomo]           


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad