|
Wananchi wakiutoa mwili wa marehemu Bandoma Mabele
(58) majini.
Wakati
vuguvugu la uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 likiwa bichi, baadhi ya sehemu zikiwa
zinasubiri zoezi hilo kutokana na sababu tofauti, matukio mbalimbali, yakiwemo
ya kusikitisha, yameripotiwa.
Huku
washindi wa nafasi mbalimbali zilizokuwa zikigombewa wakisheherekea kwa namna
ya aina yake, katika Kijiji cha Mwagika, Sengerema mkoani Mwanza, kulitokea
msiba wa kusikitisha, baada ya mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, aliyetambulika
kwa jina la Bandoma Mabele (58) kufariki dunia kufuatia kuzama ndani ya maji ya
ziwa Victoria.
Kwa mujibu
wa taarifa kutoka eneo la tukio, Mabele alikuwa akisubiri kuwania nafasi hiyo
kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa, hali iliyomlazimu kuamua kwenda ziwani kuvua
kwa ajili ya kitoweo akiwa ameongozana na vijana wawili waliotajwa kwa majina
ya Paulini Ruchiri na Samweli Malulu.
Baada ya
kuingia ziwani, katika hali isiyotarajiwa, mtumbwi wao ulipata hitilafu na
kupinduka na kuwafanya watu hao watatu kuanza kupigana kuokoa maisha yao, kitu
ambacho kilimshinda mzee Mabele na hivyo kupoteza maisha.
|
No comments:
Post a Comment