![]() |
|
Akizungumza
jana Desemba 23,2014, Mwenyekiti wa Ukawa Profesa Ibrahim Lipumba akiwa na
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbrod
Slaa, alisema Kikwete anasita kumuondoa Muhongo wakati Bunge lililishatoa maazimio
ya kutaka aondolewe.
Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), umelitaka Bunge kuiwajibisha serikali ikiwa Rais
Jakaya Kikwete atashindwa kutekeleza maazimio ya Bunge ikiwemo kumng’oa Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Akizungumza Desemba 23,2014, Mwenyekiti wa Ukawa Profesa Ibrahim Lipumba akiwa na Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbrod Slaa, alisema
Kikwete anasita kumuondoa Muhongo wakati Bunge lililishatoa maazimio ya kutaka
aondolewe.
Profesa
Lipumba alisema Bunge linalowakilisha wananchi zaidi ya milioni 45 liliazimia
uteuzi wa Muhongo utenguliwe lakini rais anasema bado anachunguza.
Profesa
Lipumba alisema kama Rais Kikwete atashindwa kumwajibisha Muhongo atakuwa
ameshindwa kutekeleza moja ya maazimio ya Bunge na kwamba Ukawa litaliomba
Bunge kuiwajibisha serikali.
Alisema moja
ya njia ya kuiwajibisha serikali ni pamoja na wabunge kupiga kura ya kutokuwa
na imani na waziri mkuu.
Profesa
Lipumba alisema “ hivi rais anachunguza nini haliamini bunge, kama anavyoteua
mawaziri pia ana madaraka ya kutengua nafasi zao, sasa anasita nini
wakati ni azimio la bunge limemwelekeza, ikumbukwe kuwa bunge kwa niaba ya
wananchi ndilo lenye jukumu la kuisimamia serikali,” - alisema Lipumba.
Alisema
hotuba aliyoitoa Jumatatu wakati akiwahutubia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam,
haijakidhi matarajio ya wengi kwani kuna maazimio hayajatekelezwa.
Azimio
ambalo halijatekelezwa na rais Kikwete ni lile linalotaka kutaifishwa kwa
mitambo ya IPTL na kutengua uteuzi wa Muhongo.
Mwenyekiti
huyo alisema rais amekataa kutekeleza azimio la kutaka mitambo ya IPTL
itaifishwe na kutoa sababu ambazo hazina maana.
“Tangu
mitambo ya IPTL imefungwa taifa limepata hasara kubwa kwa sababu umeme unaouzwa
na ni wa gharama kubwa kuliko mitambo yoyote ya umeme inayotumika katika bara
la Afrika taifa limeingia hasara kubwa, rais aitaifishe,” alisema Profesa
Lipumba.
Alisema
katika hotuba hiyo rais alionyesha kuipendelea IPTL na kuikandamiza Tanesco
wakati akielezea kuwa fedha za Escrow zilikuwa mali ya IPTL.
Hatua za
kuchukua:-BOFYA HAPA
|
Wednesday, December 24, 2014
SAKATA LA ESCROW:- Ukawa walitaka Bunge kuiwajibisha Serikali.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment