SAKATA LA ESCROW:-Rais Kikwete atengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 22, 2014

SAKATA LA ESCROW:-Rais Kikwete atengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Rais Jakaya Kikwete ametengua nafasi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kupitia hotuba aliyotoa leo Desemba 22,2014 kuzungumzia kashfa ya upotevu wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

 Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Kikwete mbele ya wazee wa Dar Es Salaam aliokuwa akiongea nao na matangazo kurushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa na vyombo vingine.

Uchunguzi uliofanywa na kamati ya hesabu za umma ya Tanzania (PAC), ilidai kuwa Profesa Tibaijuka ni mmoja wa watu walionufaika kinyume cha sheria kwa kupata fedha zilizotoka katika akauti hiyo iliyofunguliwa kutunza fedha kusubiri ufumbuzi wa mgogoro wa kibiashara kati ya kampuni ya kusambaza umeme TANESCO na kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Siku chache zilizopita Profesa Anna Tibaijuja (pichani) aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kubainisha kuwa hakuwa akikusudia kujiuzulu kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Hata hivyo Rais Kikwete hakutangaza kuwachukulia hatua watumishi wengine waliodaiwa kuhusika na tuhuma hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi zaidi unatakiwa kwa kila mtuhumiwa.

Kumekuwa na ubishi mkubwa kujadili endapo fedha ambazo ni mabilioni zilizochukuliwa zilikuwa za umma au la. Na hata Rais Kikwete amesema maelezo aliyopewa na wataalam yanaonyesha hazikuwa mali ya TANESCO.



HII NI SEHEMU TU YA HOTUBA YA RAIS KIKWETE LEO DESEMBA 22,2014.

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Anasema zoezi lilikwenda ingawa kulikuwa na dosari kadhaa

Anapongeza vyama vya siasa na wagombea na walioshinda,wafanye mikakati ya kuwaongoza wananchi

Anamuunga mkono  Waziri Hawa Ghasia kuwafukuza,kuwasimamisha kazi na kuwaonya waliovuruga uchaguzi,kwamba watumishi wa Umma sharti wawajibishwe wanaposhindwa kusimamia majukumu yao.

Vurugu wakati wa uchaguzi kuwa waliofanya vitendo vya uvunjaji wa sheria wakamatwe na kuchukuliwa hatua

Kwamba inawakatisha tamaa watu wema mhalifu akikamatwa na kuachiwa baada ya muda mfupi bila hatua kuchukuliwa

KASHIFA YA AKAUNTI YA ESCROW

Kwamba jambo la pili linalofuata sio jema masikioni mwao

Anaanza kueleza mwanzo wa sakata lilivyoibuka Bungeni

Kwamba Serikali ilihaidi na kumtaka Mkaguzi wa Serikali kukagua,na kuiagiza TAKUKURU kuchunguza  mwenendo wa miamala na hatua zichukuliwe kwa mujibu wa mamlaka waliyonayo na kuwa yoote mawili yaliyohaidiwa na Serikali yalifanyika na taarifa ya CAG iliwasilishwa Bungeni,kuwa ni zama za ukweli na uwazi aliagiza pia taarifa ichapishwe kwenye vyombo vya habari ili wananchi waifahamau.

Tarehe 8/Des/2014 baadaya ya kurudi nchini alisema ya Dodoma atayafahamu baadaye kwamba baadhi ya magazeti yalimkariri akisema akwepa ESCROW kiaina.

Baada ya kuletewa taarifa alianzakuisoma na kutoa maagizo ya ufuatiliaji ili kujua ukweli na kuwa baadhi zinaendelea kufanyiwa kazi kupata ukweli na ameamua kuzungumza ili kupunguza joto lililopo kuhusu sakata hilo

Kwamba kuna mambo manne muhimu

AKAUNT

MMILIKI

KODI ZA SERIKALI

TUHUMA ZA RUSHWA

1.AKAUNTI YA ESCROW

 kwamba kuna mkataba wa tozo la umeme'capital charge' na

2.Tozo ya uwekezaji'Capacity charges'

Katika mikataba hiyo yapo makubaliano kama utatokea mzozo,upo utaratibu uliowekwa kushughulikia tofauti inayohusu migogoro ya kiuwekezaji

1998 Tanesco na IPTL walifikishana mahakamani Tanesco ikilalamika kuwa kwenye tozo IPTL inawatoza gharama kubwa kuliko uwekezaji waliofanya mashauri endelea mpaka 2001.Katika uamuzi mahakama ilikubali malalamiko ya Tanesco na ikafanya uamuzi wa kupunguza tozo ya uwekezaji iliyotozwa na IPTL

Baadaye tanesco wakaanza vurugu kuwa wanaweza kupata punguzo zaidi,kuwa katika ukokotoaji wa kiwango cha tozo sio sawa na kuamua kutafuta nafuuu zaidi na kukubaliana maadamu kuna mzozo,tuanishe akaunti ya ESCROW na ifunguliwe Benki Kuu na wakaingia Mkataba Wizara kwa Niaba ya Tanesco na IPTL na Benki Kuu kama wakala katika Mkataba huo.

Masharti ya Akaunti kuwa bado kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake Tanesco ya Tozo na Tanesco itaendelea kulipa madai wanayopelekewa,na malipo hayo yapelekwe ESCROW Akaunti mpaka tofauti zitakapoisha na fedha kutolewa kwa muhusika.5/JULAI/2006 Akaunti ilifunguliwa

Kwamba mgogoro umekaa miaka saba bila kupata suluhisho  na katika kipindi hicho Tanesco iliendelea kulipa

Kwa mujibu wa TAARIFA YA CAG tarehe 20/Novemba/2014 akaunti ilikuwa na zaidi ya Bilioni nane kwamba kwa fedha ya Tz ilikuwa nu  202.9 bilioni

Kwa mujibu wa mkataba wa kununua umeme Tnesco isipolipa inatozwa riba ya asilimia mbili na ilikuwa inadaiwa na IPTL

Kwamba kwa mujibu wa taarifa alizopata na maelezo aliyotoa inasaidia kuweka kumbukumbu sahihi anasisitiza hadi taarifa ya CAG inatolewa zilikuwa 202bilioni  ndizo zilikuwa katika akaunti na sio306 bilioni kama zinazvyoelezwa na watu wengine

Kwamba ni matumaini yake maelezo hayo yanasaidia kupata jibu la swali maarufu kuwa fedha za nani za Umma au IPTL

AKAUNTI YA ESCROW NI NINI?

Kwamba ni tofauti na akaunti nyingine zote ambayo ni maalumu inayonzishwa kwa sababu maalumu,kufanya kazi maalumu,mashart maalumu na kazi ikiisha akaunti hiyo hufungwa

Kwamna husimamiwa na wakala aliyekubaliwa na pande zote,ndiye mwenye jukumu la kuisimamia na kumlipa mwenye fedha wakati ukifika

Kuwa Akaunti ilianzishwa na Tanesco na IPTL na Benki ku ikawa Wakala na kutoa nafasi ya pande husika kushughulikia tofauti zao

Kimsingi fedha ni mali ya IPTL kwani ndiye mlipwaji kwa kuidai Tanesco kuhusu tozo la uwekezaji

Katika swali la fedha za umma,mdhibiti alipulizwa alisema inawezekana zipo na Umma na IPTL

Mkaguzi Aliposema inawezekanakuna fedha za umma maanayake kama mgogoro ungetatuliwa na kama madai ya Tanesco yangekubaliwa kuna fedha ya Tanesco ambayo wangerudishiwa  na kuwa bahati mabay miaka saba halikufanyika na baadaye kutekelezwa uamuzi wa kufungwa akaunti na IPTL ipewe fedha yake.

Maana nyingne kwamba kuna kodi ya Serikali,Taarifa ya CAG kwamba kulikuwa na kodi ambayo haikulipwa,ambazo ni bilioni 21.7 ,Kuwa TRA ilipeleka madai yake kwa PAP kutaka ilipwe na kuwa hakuna haki ya fedha ya Tanesco

Katika ukaguzi wa hesabu za Tanesco mwaka 2012 CAG  aliwaelekeza kuacha kuhesabu fedha za akaunti ya Escrow kama fedha yao,kuwa hata kama mwenyewe alikuwa ajazichukua hizo hazikuwa zao na kuwa fedha hizo hazikuwa na sifa ya kutafsiliwa kama fedha za Tanesco

Kwamba  5/Des/2013 Mahakama  ilitoa uamuzi wa suala hilo

Kwamba Mjadala kuhusu Escrow uliibuka Serikalini  kuhusu fedha zilizopo kuhusu fedha zitoke au zibaki,Nishati walimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alishauri kutekelezwa kwa uamuzi wa Mahakama kuu

Kwamba Benki kuu nao walifuata ushauri wa Mwanasheria Mkuu ambaye alisema pia hakuna kodi ya kulipwa na kwa kuzingatia ushauri huo Akaunti ilifungwa na fedha kupewa IPTL

KUWA BAADA YA HAPO MJADALA ULIHAMIA KWENYE BUNGE NA MITANDAO YA kIJAMII kuwa imeibuka kashifa kubwa kuhus fedha hiyo

Uamuzi ule ulitiliwa shaka kuwa haukuwa sahihi na kuonekana umeitia nchi hasara na kuibua hisia kwamba sio bure kuna namna ya kuwepo mazingira ya rushwa na watu kunufaika binafsi kila mmoja akisema mambo yake,kila na kurushiana lawama za fulani kala fedha,kuwa fedha zimebebwa kwenye viroba,sandarusi,rumbesa lakini jambo moja

Alipokutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata maoni yake  alisema hakukosea katika ushauri wake  na uamuzi wa mahakama ilikuwa sahihi

Kwamba hakuna hasara iliyokuwa imepatikana kwa kuwa ililipwa kwa mtu sahihi na kuwa Akaunti hiyo ilianzishwa kutunza fedha za tozo za uwekezaji kwa IPTL

Kuwa KUWEPO KWA aKAUNTI YA ESCROW hakubadili kuwepo kwa mwenye fedha zake ambaye ni IPTL  anasisitiza Taifa halikupata hasara

Kuwa Mwanasheria alimwambia hakuna Kodi ya Serikali na kama mamlaka husika inaona kuna kodi ya kulipwa waendelee kufuatilia

Anasema hili sakata lina vurugu nyingi.

Anasema kuwa hata Umiliki wa kampuni wa PAP ulianza kutiliwa shaka

Anafafanua kuhusu makampuni yanayohusika katika sakata hili na uhalali wa kuuziana hisa na kuwa haikuwa lazima mamlaka nyingine za Serikali kufahamu

TUHUMA ZA RUSHWA KATIKA MCHAKATO

Kuwa wamesikia mengi na yataendelea kuwepo na yameandikwa mengi na mengine bado hawjayasoma kuwa rushwa ni tendo la jinai na kuwa taarifa za haruz ya rushwa aliagiza zipelekwe TAKUKURU,kuwa kuna yaliyobainika na kupewa taarifa ya awali na kuagiza yafanyiwe uchunguzi zaidi

Kwamba miamala kwenye Akaunti ya Escrow kwenye Benki ya Mkombozi kuwa Serikali inahusika na Watumishi wa Umma,na hivyo uchunguzi hautawahusu Rugemalila na watu wengine walioko nje ya Utumishi wa Umma,kuwa TAKUKURU na Tume ya Maadili itawahoji watuhumiwa

Kwamba hata waliokutwa na mamilioni kwenye akaunti zao nao watahojiwa na vyombo husika

MAAZIMIO YA BUNGE

Kuwa Serikali imeyapokea na watayafanyia kazi na wameanza kufanya hivyo na kuwapongeza Wabunge kwa moyo wa kuchukia maovu na kuwa yuko pamoja na Wabunge katika mapambano hayo

Kwamba haikuwa kazi rahisi kuwa ilikuwa kazi pevu,kuwa wamefanya kazi nzuri na mambo yameisha salama na kuwa kuna maazimio yanayozungumzika na yanayotekelezeka Anashukuru wajumbe wa Tume ya Bunge Zito Kabwe,Filikunjombe na wengine

Mwisho anapongeza michango ya wabunge na ushirikiano wa Wabunge wa CCM na Upinzani na kuwa inatakiwa kuwa hivyo katika mazingira kama hayo.

Kwamba alivyosikia upinzani wakitaka kufanya uamuzi wa Bunge kama ajenda yao binafsi na kuwa sio kweli CCM imafumbia macho wala rushwa na kuwa hata magerezani kuna wafungwa kutoka pande zote za vyama,ningeshangaa mbunge wa CCM kupinga jambo hili eti kwa ababu ya mapenzi na chama chake.

Kamati ya Bunge ilikuwa na Wabunge wa CCM wengi na kuwa kama wangeweza kukataa hoja ziziwasilishwe wangeweza kufanya hivyo kuwa sio kweli kuwa ccm haichukii rushwa

Kwamba walisema kwa uchungu juu ya uovu huo ila wapinzani wanatumia ajenda hiyo kupata sifa kwa urahisi.

Kwamba waliofanya vitendo viovu sio wenzao na CCM,kuwa bado Serikali ina dhamira ya kweli kuipinga rushwa.

1.Pendekezo la Kuchukua Mitambo ya IPTL wamelijadili na katika kipindi hiki utekelezaji wake hauwezekani hasa kulingana na ugumu wa mazingira ya utaifishaji,kuwa wawekezaji watakimbia,kwambamatatizo ya IPTL yashughulikiwe vizuri bila kujenga taswira mbaya.

2.Uwazi wa Mikataba-Hilo litafanyika na kuwa moja linahitaji muda zaidi ya kulipitia kwa kuwa kuna kanuni za usiri katika biashara ili kujiridhisha na utunzaji wa siri kama mikataba inavyotaka,kuna mambo wanaweza kukubaliana ili kulitekeleza.

3.Takukuru,Polisi wachukue hatua kwa waliotajwa kwenye Tarifa ya Kamati-Kuwa hatua zinaendelea

4.Kuwavua wadhifa Wenyeviti wa Kmati za Bunge waliotuhumiwa-Ni jukumu la Bunnge lenyewe

5.Rais kuunda Tume ya Kijaji kuchunguza majaji waliotajwa katika kashifa-Amelipokea na kulijadili kuwa namna ya utekelezaji itabidi lizingatie utaratibu wa Kikatiba na Kisheria jinsi ya kushughulikia suala hilo na kuwa sharti lianzie kwenye mahakama na sio kwa Rais.Ameachiwa Jaji Mkuu suala la Majaji

6.Kwamba Mamlaka husikika za Kifedha na Kiuchunguzi ziitaje Stanibic kujihusisha na utakatishaji wa fedha zitangazwe kama taasisi zinazotiliwa shaka-Ni pendekezo zuri kuna kitengo maalumu kilichopewa jukumu la kuchunguza ili utaratibu wa sheria uzingatiwe

7.Serikali iwasilishe mswada wa Sheria,ili Takukuru iweze kupambana na Rushwa kubwa-Kuwa mchakato wa kufanya mageuzi ndani ya Takukuru ulianza zamani na unaendelea na kuwa ni jukumu la Takukuru kupeleka mapendekezo ya mambo wanayoona yanatakiwa kufanyiwa mapendekezo.

8.Waziri wa Nishati na Madini,Waziri wa Ardhi,Bodi ya Wakurugenzi Tanesco,Katibu Mkuu Nishati wawajibishwe-Kuwa Bodi ya Tanesco imemaliza muda wake tumeanza mchakato hilo suala limejifuta lenyewe siku tano zijazo bodi,Katibu Mkuu wa Wizara tumejadili ni Mtumishi wa Umma tuhuma zake zichunguzwe kwanza ili atendewe haki,Mwanasheria ameishajiuzulu,Waziri wa Ardhi kupokea fedha kutoka VIP tumekaa na kuzungumza,Kamti ya maadili wanaendelea kuchunguza tuhuma zake,ulizwa fedha za nini amezipata kwa ajili gani,Bodi imeeleza kuwa kwa nini fedha hazikwenda kwenye shule zikaenda kwenye Akaunti yake,kuwa ni Masharti aliyopewa na mtoa fedha,kwa hiyo tumelitafakali sana kuna msingi mkubwa wa kimaadili kuna upugufu tumemuomba ajiuzulu atupe nafasi tumteue mwingine.

Waziri wa Nishati na Madini huyu tunamweka kiporo kuna uchunguzi ameagiza ufanywe hajapata majibu na baada ya uchunguzi uamuzi utafanywa kwa misingi ya Haki.

Huo ndi mwanzo na Mwisho wa Hotuba yangu ndefu,Asanteni sana


UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad