|
Dakika 10 za
kwanza za mechi ya Nani Mtani Jembe zilikuwa za hofu tupu huku wengi
wakijiuliza kama mwamuzi mwanamama kweli angeuhimili mchezo huo kutokana na
presha ilivyokuwa juu.
|
|
“Nilikimbia
huku na kule na kujikuta nikichoka ile mbaya ukizingatia hali ya hewa ya Dar ni
joto tofauti na ya Bukoba ambayo ndiyo nimeizoea.
“Jambo zuri
ni kuwa wachezaji wengi wa Yanga na Simba wanaelewa sheria za soka, hivyo
halikuwa jambo gumu kuwaelewesha.
“Jambo moja
ndilo lililoniumiza na kunichanganya, zile taarifa kuwa nilimpa Okwi kadi mara
mbili zilinishangaza sana.
“Nilianza
kupata mawazo na kuhisi familia yangu itanionaje kama ni kweli, kama ingekuwa
ni kweli basi ingehisi mtoto wao ni mbumbumbu.
“Wengi
walichanganya pale nilipompa kadi yule mchezaji namba sita (Simon Sserunkuma)
ambaye alijiangusha ndani ya eneo la penalti, kwa kuwa Okwi ni nahodha alikuja
kwangu kulalamika sasa wakadhani na kudhani kuwa niliyempa kadi ni Okwi.
“Okwi
nilikuja kumpa kadi kipindi cha pili kwa kosa la kuvuta jezi ya mpinzani wake
(Hussein Javu), hivyo nilimpa kadi ya njano moja na siyo mbili.
“Zaidi ya
hapo nashukuru Mungu sikupata vitisho vyovyote, naamini watu wengi hivi sasa
wanaufahamu mkubwa juu ya sheria 17 za soka, tofauti na zamani, ndiyo maana
sikuweza kukumbana na hali hiyo.”
Hiyo ilikuwa
mechi ya pili kubwa kwa Jonesia, ya kwanza ilikuwa ya Simba dhidi ya Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, msimu uliopita.
Katika mechi
ya Yanga, waamuzi wa pembeni walikuwa Josephat Bulali na Mohamed Mono, wote wa
Tanga.
“Mimi
sijaolewa na bado ninaishi kwetu,” alisema Jonesia huku akicheka.
Source:-
CHAMPIONI
UNGANANASI
KATIKA FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|





No comments:
Post a Comment